NENO LA LEO - JE SILAHA ZAKO ZINA UWEZO?
Tafakari: 2Wakorintho 10:3-5
"Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya
mwili; maana Silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina UWEZO KATIKA
MUNGU hata kuangusha Ngome; tukiangusha Mawazo na kila kitu
kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila
FIKIRA ipate KUMTII Kristo".
Nakumbuka usemi wa marehemu Baba wa Taifa Mwalimu JK Nyerere, wakati
Raisi wa Uganda Idd Amini alipoivamia Tanzania, Baba wa Taifa alisema
"Nia tunayo, Sababu tunayo na Uwezo wa kumpiga tunao". Ndipo akatoa Amri
ya Kumpiga na Kuivunjilia mbali ngome yake katika nchi yake.
Katika ulimwengu wetu huu uliotekwa na Adui shetani, ni jambo la kawaida
kusikia Watu wanajiita ni Wakristo, wengine wanajiita wacha Mungu,
wengine wameokoka n.k. Wanauwezo mkubwa hata wa kuimba nyimbo za dini
kwa hisia kubwa, lakini jambo la kushangaza, asilimia kubwa unawakuta
bado ni watumwa wa yule Adui.
Mbali na kuonekana watu wema au
wacha Mungu machoni pa watu, ndani ya Mawazo yao au Fikira zao, kumejaa
Visasi, Uadui, Kutosamehe, Husuda, Wivu. Wakati mawazo, maneno na
matendo ya Ngono na Mapenzi yakiendelea kukamata akili za Vijana kwa
Wazee, wakipigwa upofu wasione kuwa ni dhambi; Mungu anazidi kutoa wito
wa Kushinda vita.
Wapendwa Ngome kuu za Shetani ziko katika
MAWAZO au FIKIRA, huko ndiko zinatakiwa zivunjiliwe mbali, hatimaye
mawazo yetu yaunganishwe na Kristo. Hayo yanawezekana tu kwa watu ambao
wameruhusu utawala wa Ufalme wa Mungu kuwa ndani yao, kwa njia ya Roho
mtakatifu.
Ni wakati wa kila mmoja kujipima, kuwa je; ni kweli
amezivaa Silaha zenye Uwezo wa Mungu? Mawazo na Fikira Je zinapatana na
Mungu au zimejaa Uchafu wa yule Adui shetani? Yesu Kristo alikuja kwa
ajili ya kutuokoa kutoka katika mateka ya dhambi, na huu ndio uhuru wa
Kweli.
NAWATAKIA WOTE SIKU NJEMA YENYE BARAKA TELE NA MAFANIKIO KATIKA MWILI NA ROHO.
Friday, November 27, 2015
Tuesday, November 17, 2015
Mwanamke wa Ufunuo 17 ni Kanisa la Rumi
Mwanamke wa Ufunuo 17 ni Kanisa la Rumi
TUWEKE
kumbukumbu zetu makini zaidi.
Feburuari 26 mwaka 2009,William Shao aliandika
katika Gazeti la Rai,kwamba mwanamke anayefanana na Yule wa Ufunuo wa Yohana
17:3-11, amejemgewa sanamu mbele ya Jengo la Bunge la Umoja wa Ulaya, huko
Brussels,Ubelgiji.
Shao,
alienda mbali zaidi kusema, hata jingo lenyewe la Bunge la Ulaya(EU) mjini
Brussels, halina tofauti sana taswira yake na Mnara wa Babeli.
Shao, anasema sanamu ya mwanmke aliyeketi juu ya mnyama mbele ya ofisi za Bunge la Ulaya, haikuwekwa kwa bahati mbaya; inatafsiri jambo fulani muhimu wewe kuelewa.
Ulaya, ilikuwa himaya ya Dola ya Rumi; na
Mwanamke huyo wa mjini Brussels anayeitwa, “Europa Goddes” ni mungu mke wa
Ulaya.
Naam, mungu jike wa Ulaya ndiye mtawala wa
Ulaya na makoloni yake duniani, na mji anaoketi huitwa kwa Jina la Siri, “Babeli”
Ufunuo 17:5!!
Umeona picha
ya mnara wa Babeli? Ni kama alivyosema mwandishi William Shao,kwamba inafanana
sana na jingo la Bunge huko la Ulaya huko mjini Brussels, Ubelgiji.
‘Uropa Goddes’-mungu
jike wa Ulaya,hufananishwa na jiji la kale sana Babeli ambayo ni Irak ya siku
hizi.
Kulingana na Biblia, mwanamke katika Unabii ni
kundi la waabuduo-kanisa, waumini. Kuna wanawake wawili katika Ufunuo wa
Yohana, Ufunuo 12 na 17; moja huwakilisha kundi nyoofu katika maadili ya kidini
na, mwanamke wa Ufunuo 17 ni kundi kengeufu linalojichanganya na waabudu
sanamu, anasa za dunia na uchafu wa kiroho.
Katika Hosea
2:10,Yeremia 3:14 na 2Korintho 11:2 uhusiano baina ya Mungu Mwenyezi na Kanisa
lake hufananishwa na uhusiano wa ndoa,kati ya mume na mke.
Katika
Ufunuo 21:2 mji wa Yerusalem umefananishwa na ‘Bibi Harusi’ yaani mwanamke
safi. Kanisa la Mungu linapoungana na dunia na anasa na kuabudu sanamu,
hufananishwa na UZINZI(Tazama Yakobo 4:4).
Naam, Yakobo
anawaita watu wa Mungu waliomwacha na kuungana na Dunia ya dhambi kwamba ni
Wazinzi, waasherati, makahaba!
Ni hapa, tunapomaizi kwamba mwanamke wa Ufunuo
17:3 ambaye ni “mungu-jike wa Ulaya” ni Kanisa la Mungu lililoungana na Dunia
na mivuto yake na anasa zake na kumwacha Mungu.
Anasa,ulevi,falsafa,ibada
ya sanamu na miungu,ushoga,ulawiti hata wa watoto chekechea n.k
Mavazi ya ‘Mwanamke’
huyo ni rangi nyekundu na zambarau, ambayo yalivaliwa na makuhani wa miungu
huko Babeli ya kale.
Hawa ni kundi tajiri wenye madini,vito vya
thamani na urembo ambalo linamvuto mkubwa kwa Wafalme wa Dunia. Kanisa hilo
linasemwa kutawala miongoni mwa wafalme wa dunia(Marais, Mawaziri Wakuu,Wafalme
n.k) yaani hubebwa na watawala wa Umoja wa Ulaya huko mjini Brussels(Tazama
Ufunuo wa Yohana 17:4-6).
Muungano
haramu wa Kanisa la Mungu na viongozi wa dunia(uzinzi) ndiyo kuungana kufanya
yaliyo kinyume na Amri 10 za Mungu. Kuungana na upagani, kuabudu sanamu na
miungu kama jua, sayari,nyota na mwezi.
Mwanamke wa
mjini Brussels anao watoto wake nao ni ‘Makahaba’ yaani wazinzi wa kiroho.
Sasa,
tutazame kwa makini; kama mji wa Brussels mwaka 96 AD wakati Mtume Yohana
anaandika kitabu cha Ufunuo,ulikuwepo? Hasha!!
Nchi nzima ya Ubelgiji ina watu wasiozidi milioni
12. Brussels siku hizi una wakazi milioni 1.5 tu.
Tuutafute
mji wa kale sana Ulaya, ambao Yohana aliuita jina la mafumbo Babeli. Umejengwa
juu ya milima saba(ufunuo 17:9).
Mwaka 753 BC mji uliojengwa Ulaya ni Rome.
Hata London haukuwepo, Uingereza ilikuwa kijiji kidogo mwaka 1000 AD. Hata
mwaka 500 BC Rome lilikuwa jiji tena “SUPER POWER” Duniani, ulijengwa na
Romulus.
Katika mji huu ndiko yaliko mamlaka ya
kidini,Vatican. Unaposema Vatican unasema kanisa la Mungu. Vatican imekuwa nchi
Feburuari 11, mwaka 1929 zama za Benito Mussolini.
Rome ni
mahali ambapo wameishi ma-Baba Watakatifu(Popes) wa Katoliki wapatao 302. Mji
huu ulikuwa makao makuu ya dola ya Rumi, hata zama za Yesu,mitume na zama za
Biblia Takatifu yaani kati ya mwaka BC 1500 ZAMA ZA MUSA Hadi 96 AD alipofariki
Yohana wa Patmo.
Nataka msomaji atambue kwamba, waandishi wa
Biblia waliposema Babeli,baada ya kuanguka kwa mji wa Babeli, walimaanisha MJI
WA ROME(Isaya 21:9).
Fahari yake
na ulikuwa mji mkuu wa biashara duniani. Kanisa Katoliki linadai Petro
aliyefika mjini Rome mwaka 42 AD na akauliwa na Kaisari Nero Mkatili, mwaka AD
67,ndiye Papa wa Kwanza kwa Kanisa hilo.
Tuwatazame mapapa. Huchaguliwa na Makadinari
kama 131 hivi. Papa Benedict XVI yeye alichaguliwa na Makadinali 117, ambao
hawakuwa na umri wa miaka 80. Papa ni Mwakilishi wa Yesu,mrithi wa Mtume
Petro,Mkuu wa Mitume wote duniani,Papa ni Mamlaka na nguvu-Tazama Danieli 7:25.
Rome, ni mahali Kanisa la Mt.Petro
lilipojengwa juu ya Kanisa la Petro; linaitwa, St.Peter’s Basilica. Limejengwa KATIKA
ENEO LA EKARI SITA.
Hili kanisa,
St. Peter’s Basilica, lina urefu wa futi 700 na upana ni futi 450 na linaweza
kuchukua watu 80,000 kwa wakati mmoja.
Rome ni jiji
lililopo nyuzi sawa na New York kwa nyuzi za Latitude; ni jiji lenye Coliseum,
ambamo yalifugwa masimba yaliyorarua Wakristo maelfu.
Rome,uko
futi 40 hadi 270 juu ya usawa wa Bahari. Jiji lenye kelele nyingi kuliko mji
wowote duniani,lipo kando ya Bahari ya Mediterranean.
Zama za Papa Pius XII alibebwa kwenye kiti cha
enzi kiitwacho, Sedia Gastatoria ambacho
ni kiti cha enzi cha dhahabu chenye rangi nyekundu.Papa huketi hapa mara
anapochaguliwa na Moshi Mweupe, hutoa
BARAKA Duniani- Urbi et Orbi.
Rome
umejengwa juu ya milima saba: CAPITALINE, PALATINE, AVENTINE, QUIRINAL, VIMINAL,
ESQUILINE, na CAELIAN.
Hapa, ndipo
liketipo kanisa lile la Mungu ambalo sasa linataka kugeuka kuwa kama Yule mama
wa mjini Brussels.
Mwanamke
huyu ni kanisa. Kanisa linapoungana na dunia na kuacha usafi wa kiroho huitwa, ‘BABELI’
ya siri iliyoanguka na Mungu huwaita watu wake watoke humo(Ufunuo 18:2-4).
Kuanguka ni
kuacha usafi wa kiroho,kumwacha Mungu na kuungana na uchafu kama unajisi,siasa
za kugombea tawala za dunia,ufisadi,mapinduzi,ulawiti,ushoga n.k
Jiji lenye
utajiri wa dhahabu na vito vya thamani lenye kuwakosesha watu kwa mafundisho
yenye kuridhia dhambi(uasi wa sheria ya Mungu) kama jambo dogo tu-Uhuru na
demokrasia,haki za binadamu n.k
Wapo
wanaofuata kila jambo na ni ‘watoto’ wa Yule mama wa mjini Brussels.
Tafakarini.
JE! NAWEZA KULIPATA KANISA LA MUNGU LEO?
JE!
NAWEZA KULIPATA KANISA
LA MUNGU LEO?
LA MUNGU LEO?

1.
Kanisa Lilianzishwa Na Yesu
Maisha
na mafundisho ya Yesu yalianzisha umoja wa imani na ushirika wa karibu
sana katika kanisa lile la mitume walilolianzisha. Mitume wale walikuwa
na uhusiano wa karibu kabisa na Kristo yule aliyefufuka. Paulo alitoa
picha ya kifungo hicho cha karibu sana na kukilinganisha na uhusiano
wa ndoa:
"Naliwaposea Mume mmoja, yaani, Kristo, ili niwalete ninyi kwake mkiwa bikira safi." - 2 Wakorintho 11:2.
"Naliwaposea Mume mmoja, yaani, Kristo, ili niwalete ninyi kwake mkiwa bikira safi." - 2 Wakorintho 11:2.
Kulingana
na maneno ya Paulo, kanisa la Kikrsto ni mwanamke safi, ni bibi-arusi
wa Kristo, ishara inayofaa kabisa kwa kanisa lake Kristo alipendalo.
Katika Agano la Kale mithali iyo hiyo inatumika kuielezea Israeli, yaani,
wateule wa Mungu. Mungu aliwaambia Israeli: "wewe kama bibi-arusi
ulinipenda mimi" (Yeremia 2:2); "Mimi ni mume wenu" (Yeremia
3:14).
Kitabu
cha Ufunuo pia kinazungumza juu ya kanisa kama mwanamke:
"Ishara kuu na ya ajabu ilionekana mbinguni: mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake" - (Ufunuo 12:1).
"Ishara kuu na ya ajabu ilionekana mbinguni: mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake" - (Ufunuo 12:1).

Mwanamke
huyo ana"mwezi chini ya miguu yake." Mwezi huo unawakilisha
nuru ya Injili iliyoakisiwa [iliyoangaza] katika dhabihu na taratibu
za ibada ya watu wa Mungu katika Agano la Kale. Mwezi huo ukiwa "chini
ya miguu yake" unadokeza kwamba nuru ya Injili iliyoakisiwa imepitwa
na huduma anayofanya Kristo.
Mwanamke
huyo anayo "taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake."
Nyota zinawakilisha vizuri sana mitume wale kumi na wawili, watu waadilifu
ambao ushuhuda wao juu ya Yesu unang'aa sana mpaka siku hii ya leo.
Ni
dhahiri, basi, kwamba maelezo yamhusuyo mwanamke huyo yanaonyesha kwamba
Yohana katika mawazo yake analiona badiliko lililotokea kutoka kwa watu
wa Mungu, Israeli, katika Agano la Kale kwenda kwenye kanisa lile la
Kikrsto la Agano Jipya alilolianzisha Yesu. Jua, mwezi, na nyota huitilia
mkazo huduma ya kupeleka nuru inayofanywa na kanisa hilo la Kikristo
kwa kuzitangaza hizo Habari Njema.
2.
Matukio Yanayofuatana Ya Kushindwa Kwa Shetani
Kuingia
kwa mwanamke huyo kunaweka jukwaa kwa matukio haya makuu yanayofuatana:
"Alikuwa mja mzito, naye akapaaza sauti kwa maumivu na uchungu wa kujifungua mtoto. Kisha, ishara nyingine ikatokea mbinguni: joka mkubwa jekundu na lenye pembe kumi na vichwa saba; na kila kichwa kilikuwa na taji. Joka hilo liliburuta kwa mkia wake theluthi moja ya nyota za anga na kuzitupa duniani. Nalo lilisimamaa mbele ya huyo mama aliyekuwa karibu kujifungua mtoto, tayari kabisa kummeza mtoto, mara tu atakapozaliwa. Kisha, mama huyo akajifungua mtoto wa kiume ambaye atayatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Lakini mtoto akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu na kwenye kiti chake cha enzi" - Ufunuo 12:2-5.
"Alikuwa mja mzito, naye akapaaza sauti kwa maumivu na uchungu wa kujifungua mtoto. Kisha, ishara nyingine ikatokea mbinguni: joka mkubwa jekundu na lenye pembe kumi na vichwa saba; na kila kichwa kilikuwa na taji. Joka hilo liliburuta kwa mkia wake theluthi moja ya nyota za anga na kuzitupa duniani. Nalo lilisimamaa mbele ya huyo mama aliyekuwa karibu kujifungua mtoto, tayari kabisa kummeza mtoto, mara tu atakapozaliwa. Kisha, mama huyo akajifungua mtoto wa kiume ambaye atayatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Lakini mtoto akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu na kwenye kiti chake cha enzi" - Ufunuo 12:2-5.
Wakuu
watatu wanashiriki katika mfululizo wa matukio haya:
Mwanamke, huyo tayari ametambulishwa kama kanisa lake Mungu.
Mtoto wa kiume aliyezaliwa na mwanamke huyo ana"nyakuliwa hata kwa Mungu na kwenye kiti chake cha enzi," na siku moja "atayatawala mataifa yote." Yesu ndiye mtoto peke yake aliyepata kuzaliwa katika ulimwengu huu ambaye alinyakuliwa kwenda kwenye kiti cha enzi cha Mungu na ambaye siku moja atayatawala mataifa yote.
Joka anamwakilisha Ibilisi, au Shetani.
"Kisha
kukazukaa vita mbinguni: Mikaeli na malaika wake walipigana na hilo
joka, nalo likawashambulia pamoja na malaika wake. Lakini joka hilo
na malaika wake walishindwa, na hatimaye hapakuwa tena na nafasi mbinguni
kwa ajili yao. Basi, joka hilo kuu likatupwa nje. Joka hilo ndiye yule
nyoka wa kale ambaye huudanganya ulimwengu wote. Naam, alitupwa duniani,
na malaika wake wote pamoja naye." - Ufunuo 12:7-9.
Mwanamke, huyo tayari ametambulishwa kama kanisa lake Mungu.
Mtoto wa kiume aliyezaliwa na mwanamke huyo ana"nyakuliwa hata kwa Mungu na kwenye kiti chake cha enzi," na siku moja "atayatawala mataifa yote." Yesu ndiye mtoto peke yake aliyepata kuzaliwa katika ulimwengu huu ambaye alinyakuliwa kwenda kwenye kiti cha enzi cha Mungu na ambaye siku moja atayatawala mataifa yote.
Joka anamwakilisha Ibilisi, au Shetani.

Picha
hiyo inakuwa dhahiri mara tu tunapoifahamu mifano hiyo. Ibilisi na malaika
zake "wa[lipo] poteza mahali pao mbinguni," wali"tupwa
duniani." Yesu alipozaliwa katika dunia hii, Ibilisi alijaribu
kumwua Yesu, mwana yule wa kiume, mara tu alipokwisha kuzaliwa. Alishindwa,
kisha Yesu "akanyakuliwa" kwenda kwenye kiti cha enzi cha
Mungu.
Ndipo
Shetani akaondoka kwenda kuliangamiza kabisa kanisa la Kristo alilolianzisha
Kristo. Mtume Yohana, aliyekiandika kitabu cha Ufunuo, aliliona kidogo
tu pambano hilo kuu kati ya Kristo na Shetani likipiganwa vikali sana
juu ya dunia hii. Vita hiyo ilipofikia kilele chake wakati ule wa kusulibiwa
kwake Kristo, Yohana alisikia sauti ikipiga kelele kutoka mbinguni,
ikisema:
"Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikisema: Sasa umefikia mkombozi na nguvu na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake! Maana yule aliyewashtaki ndugu zetu mbele ya Mungu ametupwa chini. Naam, ametupwa chini huyo anayewashtaki usiku na mchana"- Ufunuo 12:10. (Linganisha na Yohana 12:31 na Luka 10:18).
"Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikisema: Sasa umefikia mkombozi na nguvu na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake! Maana yule aliyewashtaki ndugu zetu mbele ya Mungu ametupwa chini. Naam, ametupwa chini huyo anayewashtaki usiku na mchana"- Ufunuo 12:10. (Linganisha na Yohana 12:31 na Luka 10:18).

"Sasa
umekuja wokovu" ni tangazo linaloonyesha kwamba tendo lile la kilele
la historia limefika. Kuzaliwa kwake Kristo, Mwokozi wa ulimwengu, kumekwisha
kutokea (fungu la 5). Licha ya majaribu makali ya Shetani, Yesu aliishi
maisha yasiyo na dhambi, alikufa na kufufuka akiwa mshindi dhidi ya
dhambi na mauti (fungu la 10). Shetani ameshindwa milele (fungu la 7-9).
Msalaba umetukuzwa katika uwezo wake wote.
Tangazo
hili, "Sasa umekuja wokovu," halimpendezi Yohana tu, bali
malimwengu yote:
"Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, na ninyi mkaao humo! Ole kwa nchi na bahari, kwa sababu Ibilisi ameshuka kuja kwenu! Amejaa ghadhabu nyingi, kwa sababu anajua kwamba ana wakati mchache tu." - (Ufunuo 12:12).
"Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, na ninyi mkaao humo! Ole kwa nchi na bahari, kwa sababu Ibilisi ameshuka kuja kwenu! Amejaa ghadhabu nyingi, kwa sababu anajua kwamba ana wakati mchache tu." - (Ufunuo 12:12).
Mbingu
yote ilisherehekea ushindi wa Kristo. Kristo aliyavunjilia mbali madai
ya aina yo yote ile aliyokuwa nayo Shetani zamani kuhusu kuwa na mahali
pake kule mbinguni, na yule Shetani aliyeshindwa akapoteza milele madai
yake aliyosema dunia hii ni yake.
3.
Kanisa La Kikristo Katika Mapambano Dhidi Ya Shetani
Kabla
Yesu hajapaa kwenda mbinguni alilianzisha kanisa la Kikristo (ambalo
linafananishwa na mwanamke). Kifo chake pale msalabani kililipa hilo
kanisa la Kikristo uwezo wa kumshinda Shetani.
"Nao
[Kanisa la Kikristo] wakamshinda [Shetani] kwa damu ya Mwana-Kondoo
na kwa neno la ushuhuda wao; hawakuyapenda sana maisha yao kiasi cha
kuogopa kufa." - (Ufunuo 12:11).

"Wakamshinda [Shetani] kwa damu ya Mwana-Kondoo." Yesu alinyakuliwa hadi kwenye kiti cha enzi cha Mungu ili apate kuifanya damu yake iwe na matokeo mema katika maisha ya wafuasi wake. Yeye anaweza kuiondoa kumbukumbu ya dhambi zetu, anaweza kutuokoa kwa njia ya damu yake iliyomwagika (1Yohana 1:7), na kutupa uwezo wa kuishi maisha yenye afya ya Kikristo siku kwa siku.
"Hawakuyapenda sana maisha yao kiasi cha kuogopa kufa." "Damu ya Mwana-Kondoo" iliwafanya wawe tayari kufa kwa ajili ya kazi yake Kristo; hawa"kuogopa kufa." Mungu alikuwa ameteseka sana,kwa hivyo Wakristo wale wafia dini walikuwa tayari kuteswa na kuuawa. Hata watoto wadogo walijitoa mhanga hatimaye. Kisa kinasimuliwa cha mama mmoja Mkristo aliyetupwa kwa Simba katika uwanja wa michezo wa Kiroma kwa kuwa alitoa utii wake kwa Kristo, wala si kwa serikali. Binti yake mdogo,
badala ya kujikunyata kwa hofu kuu, alisikia ari ya kujitoa wakfu ikijaa ndani yake. Wale simba walipomshambulia mama yake, alisimama na kupiga kelele, "Mimi pia ni Mkristo." Maafisa wa Kiroma wakamkamata na kumtupa kwa nguvu kwa wanyama wale wenye njaa.

Ufunuo
12:11 huonyesha picha ya kanisa linaloshinda ambalo limejaa washindi:
mitume, wafia dini, wanamatengenezo ya kanisa, na Wakristo wengineo
waaminifu. Upole, uaminifu, ujasiri, na ushindi wao umenguruma kushuka
katika karne nyingi na kuupindua ulimwengu.
Kwa
kuwa Shetani alishindwa kumwangamiza Yesu alipoishi hapa duniani, sasa
anajitahidi sana kumwangamiza Kristo anayeishi ndani ya kanisa lake.
"Joka
lilipotambua kwamba limetupwa chini duniani, likaanza kumwinda yule
mama aliyekuwa amejifungua mtoto wa kiume. Lakini mama huyo akapewa
mabawa mawili ya tai apate kuruka mbali sana na hilo joka, mpaka mahali
pake jangwani ambapo angehifadhiwa salama kwa muda wa miaka mitatu na
nusu. Basi, joka likatapika maji mengi kama mto, yakamfuata huyo mama
nyuma ili yamchukue. Lakini nchi ikamsaidia huyo mama: ikajifunua kama
mdomo na kuyamezaaa maji hayo yaliyotoka kinywani mwa hilo joka - (Ufunuo
12:13-16).

Akiwa
amekasirika vibaya sana dhidi ya kushindwa kwake pale msalabani, Shetani
akaielekeza ghadhabu yake dhidi ya Kanisa lile alilolianzisha Yesu.
Katika miongo [miaka kumi-kumi] iliyofuata baada ya kusulibiwa kwake
Kristo, maelfu waliuawa katika ule uwanja wa duara uliojengwa mjini
Roma (Colosseum), maeneo tupu ya pembe mraba yaliyokuwa mijini, magereza
yale ya chini ya ardhi, na katika maficho ya jangwani.
Mwanzoni
wale wenye mamlaka [serikali] ya kidunia walianzisha hayo mateso. Lakini
baada ya kufa wale mitume badiliko lilitokea taratibu ndani ya kanisa
lile. Katika kipindi kile cha karne ya pili, ya tatu, na ya nne, wengi
ndani ya kanisa lile walianza kuzibadili kidogo zile kweli zilizokuwa
zimefundishwa na Kristo pamoja na mitume wake. Viongozi fulani, walioasi
hata wakaanza kuwatesa Wakristo wale waliosisitiza kuwa na usafi wa
itikadi [imani] za Agano Jipya.
Wataalam
wa Biblia wanakadiria kwamba takriban milioni 50 ya wale waliokuwa waaminifu
waliuawa. Katika jitihada yake ya kulizamisha na kuliangamiza kanisa,
Ibilisi alitoa "mto" wa mateso ili kulifanya "lichukuliwe
[lile kanisa] na mkondo ule wa mto." "Lakini nchi ikamsaidia
yule mwanamke kwa… kuumeza ule mto" wa mateso na mafundisho
ya uongo.
Katika
kipindi cha mateso ya Zama za Kati [1100-1500], kanisa la kweli lilijiondoa
kutoka katika uongozi ule ulioasi na kujificha "Nyikani, mahali
alipoandaliwa na Mungu, ili wamlishe muda wa siku 1,260" (fungu
la 6). Utabiri huo ulitimizwa katika kipindi cha miaka 1260 ya mateso
kuanzia mwaka wa 538 hadi mwaka wa 1798 B.K. (siku moja mara nyingi
husimama badala ya mwaka mmoja katika unabii wa mifano wa Biblia, angalia
Ezekieli 4:6).
Katika
kipindi cha karne za giza Wakristo waaminifu walioiamini Biblia walipata
kimbilio lao po pote walipoweza kupapata kwa mfano, katika mabonde ya
Wawaldensia wa Italia magharibi na Ufaransa mashariki, na katika kanisa
la Kikeltiki [Waskoti Waairishi, Waweishi] la visiwa vya Uingereza.
4.
Kanisa La Mungu Katika Siku Hizi Zetu
Jambo
hilo linatufikisha katika siku hizi zetu - yaani, kwenye kanisa la kweli
la Kristo tangu mwaka wa 1798. Kama ambavyo ingeweza kutarajiwa, yule
joka bado amewakasirikia watu wa Mungu. Vita kuu isiyoonekana kwa macho
inaendelea. Kwa kweli, Shetani anafanya shambulio lake kubwa kabisa
dhidi ya kanisa hilo muda mfupi tu kabla ya kuja kwake Yesu.
"Ndipo
yule Joka [Ibilisi] akamkasirikia sana yule mwanamke [Kanisa la Mungu],
akaenda zake afanye vita dhidi ya wazao wake waliosalia - wale wanaozitii
amri za Mungu na kuwa na ushuhuda wa Yesu." - (Ufunuo 12:17).
Unabii
huu unalenga katika siku zetu hizi. Shetani amekasirika sana; anafanya
vita dhidi ya wazao wa mwanamke waliosalia" - yaani, dhidi ya watu
wa Mungu wa siku hizi. Angalia alama zao zinazowatambulisha:
(1)Waumini
hao wa siku za mwisho wanao "ushuhuda wa Yesu." Kwa uaminifu
wakiyang'ang'ania mafundisho safi ya Neno la Mungu, wanamshuhudia Yesu
kwa njia ya maisha yao yenye nguvu nyingi ya Kikristo.

(2)
Wakristo hao wa siku za mwisho ni watu wa unabii. Kuupokea ule "ushuhuda
wa Yesu Kristo" kulimwezesha Yohana kukiandika kitabu kile cha
Ufunuo (Ufunuo 1:1-3). Kundi hilo la mwisho la waumini linapokea karama
ile ile: yaani, ushuhuda wa moja kwa moja toka kwa Mungu kupitia kwa
mjumbe wa kibinadamu. Karama yao ya unabii inalenga juu ya ufunuo wa
Mungu kuhusu utume wao na mwisho wao.
(3)
Wakristo hao wa siku hizi za mwisho wanatambulikana pia kama "wale
wanaozitii Amri [kumi] za Mungu." Hawatetei tu ukamilifu wa hizo
Amri Kumi, bali wanazitii pia. Upendo wa Mugu ulio mioyoni mwao unawaletea
utii unaotolewa kwa moyo wa furaha (Warumi 5:5; 13:8-10).
Wakristo
hao wa siku hizi za mwisho wanakifuata kielelezo cha Kristo na cha kanisa
lile la kwanza kwa kuzitii amri [kumi] za Mungu. Jambo hilo linamkasirisha
vibaya sana yule Joka - yaani, yule Ibilisi. Naye anapigana vita dhidi
ya "wazao" wa mwanamke "waliosalia" kwa sababu wanatoa
ushuhuda kwamba upendo wao kwa Mungu unawafanya wafuasi wake hao kuwa
watii. Kama vile Kristo alivyoagiza, aliposema:
"Mkinipenda, mtazishika amri zangu" - Yohana 14:15.
"Mkinipenda, mtazishika amri zangu" - Yohana 14:15.
Maisha
ya Wakristo hao wa siku hizi za mwisho yanaonyesha kwamba uwezekano
upo wa kumpenda Mungu kwa mioyo yetu yote na kuwapenda wenzetu kama
sisi tunavyojipenda wenyewe. Kulingana na maneno ya Yesu, sifa hizo
za tabia, yaani, upendo kwa Mungu na upendo kwa watu, hufanya muhtasari
wa Amri kumi za Mungu (Mathayo 22:35-40).
Ya
nne katika hizo amri inatutaka sisi kuitunza Jumamosi, siku ya saba
ya juma, kama Sabato. Kwa kuwa upendo wao kwa Yesu umezitia ndani ya
mioyo yao amri zote kumi [Ebr. 8:10; Kut. 20:3-17; Yak. 2:10-12], basi,
Wakristo hao wa siku hizi za mwisho ni Wasabato.
Sabato
ndicho kiini cha ujumbe wa mwisho wa Mungu kwa watu wake katika kitabu
cha Ufunuo, sura ya 12 na 14:6-15. Nguvu zote za mbinguni zinajipanga
nyuma ya Wakristo hao wa siku hizi za mwisho walioelezwa katika sura
hizo. Mwokozi wao aliye hai ndiye rafiki yao daima, na Roho Mtakatifu
anafanya kazi yake "kuwafanya imara kwa nguvu katika utu wao wa
ndani." Ahadi yake ni ya hakika. WATAmshinda Shetani "kwa
damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao" (Ufunuo 12:11).
Je!
unataka kuwa mmoja wa Wakristo hao wa siku hizi za mwisho ambao "wanazitii
amri [kumi] za Mungu" tena wa"na ushuhuda wa Yesu"? Kwa
nini usikate shauri sasa hivi?
Subscribe to:
Posts (Atom)