JE!
NAWEZA KULIPATA KANISA
LA MUNGU LEO?
LA MUNGU LEO?

1.
Kanisa Lilianzishwa Na Yesu
Maisha
na mafundisho ya Yesu yalianzisha umoja wa imani na ushirika wa karibu
sana katika kanisa lile la mitume walilolianzisha. Mitume wale walikuwa
na uhusiano wa karibu kabisa na Kristo yule aliyefufuka. Paulo alitoa
picha ya kifungo hicho cha karibu sana na kukilinganisha na uhusiano
wa ndoa:
"Naliwaposea Mume mmoja, yaani, Kristo, ili niwalete ninyi kwake mkiwa bikira safi." - 2 Wakorintho 11:2.
"Naliwaposea Mume mmoja, yaani, Kristo, ili niwalete ninyi kwake mkiwa bikira safi." - 2 Wakorintho 11:2.
Kulingana
na maneno ya Paulo, kanisa la Kikrsto ni mwanamke safi, ni bibi-arusi
wa Kristo, ishara inayofaa kabisa kwa kanisa lake Kristo alipendalo.
Katika Agano la Kale mithali iyo hiyo inatumika kuielezea Israeli, yaani,
wateule wa Mungu. Mungu aliwaambia Israeli: "wewe kama bibi-arusi
ulinipenda mimi" (Yeremia 2:2); "Mimi ni mume wenu" (Yeremia
3:14).
Kitabu
cha Ufunuo pia kinazungumza juu ya kanisa kama mwanamke:
"Ishara kuu na ya ajabu ilionekana mbinguni: mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake" - (Ufunuo 12:1).
"Ishara kuu na ya ajabu ilionekana mbinguni: mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake" - (Ufunuo 12:1).

Mwanamke
huyo ana"mwezi chini ya miguu yake." Mwezi huo unawakilisha
nuru ya Injili iliyoakisiwa [iliyoangaza] katika dhabihu na taratibu
za ibada ya watu wa Mungu katika Agano la Kale. Mwezi huo ukiwa "chini
ya miguu yake" unadokeza kwamba nuru ya Injili iliyoakisiwa imepitwa
na huduma anayofanya Kristo.
Mwanamke
huyo anayo "taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake."
Nyota zinawakilisha vizuri sana mitume wale kumi na wawili, watu waadilifu
ambao ushuhuda wao juu ya Yesu unang'aa sana mpaka siku hii ya leo.
Ni
dhahiri, basi, kwamba maelezo yamhusuyo mwanamke huyo yanaonyesha kwamba
Yohana katika mawazo yake analiona badiliko lililotokea kutoka kwa watu
wa Mungu, Israeli, katika Agano la Kale kwenda kwenye kanisa lile la
Kikrsto la Agano Jipya alilolianzisha Yesu. Jua, mwezi, na nyota huitilia
mkazo huduma ya kupeleka nuru inayofanywa na kanisa hilo la Kikristo
kwa kuzitangaza hizo Habari Njema.
2.
Matukio Yanayofuatana Ya Kushindwa Kwa Shetani
Kuingia
kwa mwanamke huyo kunaweka jukwaa kwa matukio haya makuu yanayofuatana:
"Alikuwa mja mzito, naye akapaaza sauti kwa maumivu na uchungu wa kujifungua mtoto. Kisha, ishara nyingine ikatokea mbinguni: joka mkubwa jekundu na lenye pembe kumi na vichwa saba; na kila kichwa kilikuwa na taji. Joka hilo liliburuta kwa mkia wake theluthi moja ya nyota za anga na kuzitupa duniani. Nalo lilisimamaa mbele ya huyo mama aliyekuwa karibu kujifungua mtoto, tayari kabisa kummeza mtoto, mara tu atakapozaliwa. Kisha, mama huyo akajifungua mtoto wa kiume ambaye atayatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Lakini mtoto akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu na kwenye kiti chake cha enzi" - Ufunuo 12:2-5.
"Alikuwa mja mzito, naye akapaaza sauti kwa maumivu na uchungu wa kujifungua mtoto. Kisha, ishara nyingine ikatokea mbinguni: joka mkubwa jekundu na lenye pembe kumi na vichwa saba; na kila kichwa kilikuwa na taji. Joka hilo liliburuta kwa mkia wake theluthi moja ya nyota za anga na kuzitupa duniani. Nalo lilisimamaa mbele ya huyo mama aliyekuwa karibu kujifungua mtoto, tayari kabisa kummeza mtoto, mara tu atakapozaliwa. Kisha, mama huyo akajifungua mtoto wa kiume ambaye atayatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Lakini mtoto akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu na kwenye kiti chake cha enzi" - Ufunuo 12:2-5.
Wakuu
watatu wanashiriki katika mfululizo wa matukio haya:
Mwanamke, huyo tayari ametambulishwa kama kanisa lake Mungu.
Mtoto wa kiume aliyezaliwa na mwanamke huyo ana"nyakuliwa hata kwa Mungu na kwenye kiti chake cha enzi," na siku moja "atayatawala mataifa yote." Yesu ndiye mtoto peke yake aliyepata kuzaliwa katika ulimwengu huu ambaye alinyakuliwa kwenda kwenye kiti cha enzi cha Mungu na ambaye siku moja atayatawala mataifa yote.
Joka anamwakilisha Ibilisi, au Shetani.
"Kisha
kukazukaa vita mbinguni: Mikaeli na malaika wake walipigana na hilo
joka, nalo likawashambulia pamoja na malaika wake. Lakini joka hilo
na malaika wake walishindwa, na hatimaye hapakuwa tena na nafasi mbinguni
kwa ajili yao. Basi, joka hilo kuu likatupwa nje. Joka hilo ndiye yule
nyoka wa kale ambaye huudanganya ulimwengu wote. Naam, alitupwa duniani,
na malaika wake wote pamoja naye." - Ufunuo 12:7-9.
Mwanamke, huyo tayari ametambulishwa kama kanisa lake Mungu.
Mtoto wa kiume aliyezaliwa na mwanamke huyo ana"nyakuliwa hata kwa Mungu na kwenye kiti chake cha enzi," na siku moja "atayatawala mataifa yote." Yesu ndiye mtoto peke yake aliyepata kuzaliwa katika ulimwengu huu ambaye alinyakuliwa kwenda kwenye kiti cha enzi cha Mungu na ambaye siku moja atayatawala mataifa yote.
Joka anamwakilisha Ibilisi, au Shetani.

Picha
hiyo inakuwa dhahiri mara tu tunapoifahamu mifano hiyo. Ibilisi na malaika
zake "wa[lipo] poteza mahali pao mbinguni," wali"tupwa
duniani." Yesu alipozaliwa katika dunia hii, Ibilisi alijaribu
kumwua Yesu, mwana yule wa kiume, mara tu alipokwisha kuzaliwa. Alishindwa,
kisha Yesu "akanyakuliwa" kwenda kwenye kiti cha enzi cha
Mungu.
Ndipo
Shetani akaondoka kwenda kuliangamiza kabisa kanisa la Kristo alilolianzisha
Kristo. Mtume Yohana, aliyekiandika kitabu cha Ufunuo, aliliona kidogo
tu pambano hilo kuu kati ya Kristo na Shetani likipiganwa vikali sana
juu ya dunia hii. Vita hiyo ilipofikia kilele chake wakati ule wa kusulibiwa
kwake Kristo, Yohana alisikia sauti ikipiga kelele kutoka mbinguni,
ikisema:
"Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikisema: Sasa umefikia mkombozi na nguvu na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake! Maana yule aliyewashtaki ndugu zetu mbele ya Mungu ametupwa chini. Naam, ametupwa chini huyo anayewashtaki usiku na mchana"- Ufunuo 12:10. (Linganisha na Yohana 12:31 na Luka 10:18).
"Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikisema: Sasa umefikia mkombozi na nguvu na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake! Maana yule aliyewashtaki ndugu zetu mbele ya Mungu ametupwa chini. Naam, ametupwa chini huyo anayewashtaki usiku na mchana"- Ufunuo 12:10. (Linganisha na Yohana 12:31 na Luka 10:18).

"Sasa
umekuja wokovu" ni tangazo linaloonyesha kwamba tendo lile la kilele
la historia limefika. Kuzaliwa kwake Kristo, Mwokozi wa ulimwengu, kumekwisha
kutokea (fungu la 5). Licha ya majaribu makali ya Shetani, Yesu aliishi
maisha yasiyo na dhambi, alikufa na kufufuka akiwa mshindi dhidi ya
dhambi na mauti (fungu la 10). Shetani ameshindwa milele (fungu la 7-9).
Msalaba umetukuzwa katika uwezo wake wote.
Tangazo
hili, "Sasa umekuja wokovu," halimpendezi Yohana tu, bali
malimwengu yote:
"Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, na ninyi mkaao humo! Ole kwa nchi na bahari, kwa sababu Ibilisi ameshuka kuja kwenu! Amejaa ghadhabu nyingi, kwa sababu anajua kwamba ana wakati mchache tu." - (Ufunuo 12:12).
"Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, na ninyi mkaao humo! Ole kwa nchi na bahari, kwa sababu Ibilisi ameshuka kuja kwenu! Amejaa ghadhabu nyingi, kwa sababu anajua kwamba ana wakati mchache tu." - (Ufunuo 12:12).
Mbingu
yote ilisherehekea ushindi wa Kristo. Kristo aliyavunjilia mbali madai
ya aina yo yote ile aliyokuwa nayo Shetani zamani kuhusu kuwa na mahali
pake kule mbinguni, na yule Shetani aliyeshindwa akapoteza milele madai
yake aliyosema dunia hii ni yake.
3.
Kanisa La Kikristo Katika Mapambano Dhidi Ya Shetani
Kabla
Yesu hajapaa kwenda mbinguni alilianzisha kanisa la Kikristo (ambalo
linafananishwa na mwanamke). Kifo chake pale msalabani kililipa hilo
kanisa la Kikristo uwezo wa kumshinda Shetani.
"Nao
[Kanisa la Kikristo] wakamshinda [Shetani] kwa damu ya Mwana-Kondoo
na kwa neno la ushuhuda wao; hawakuyapenda sana maisha yao kiasi cha
kuogopa kufa." - (Ufunuo 12:11).

"Wakamshinda [Shetani] kwa damu ya Mwana-Kondoo." Yesu alinyakuliwa hadi kwenye kiti cha enzi cha Mungu ili apate kuifanya damu yake iwe na matokeo mema katika maisha ya wafuasi wake. Yeye anaweza kuiondoa kumbukumbu ya dhambi zetu, anaweza kutuokoa kwa njia ya damu yake iliyomwagika (1Yohana 1:7), na kutupa uwezo wa kuishi maisha yenye afya ya Kikristo siku kwa siku.
"Hawakuyapenda sana maisha yao kiasi cha kuogopa kufa." "Damu ya Mwana-Kondoo" iliwafanya wawe tayari kufa kwa ajili ya kazi yake Kristo; hawa"kuogopa kufa." Mungu alikuwa ameteseka sana,kwa hivyo Wakristo wale wafia dini walikuwa tayari kuteswa na kuuawa. Hata watoto wadogo walijitoa mhanga hatimaye. Kisa kinasimuliwa cha mama mmoja Mkristo aliyetupwa kwa Simba katika uwanja wa michezo wa Kiroma kwa kuwa alitoa utii wake kwa Kristo, wala si kwa serikali. Binti yake mdogo,
badala ya kujikunyata kwa hofu kuu, alisikia ari ya kujitoa wakfu ikijaa ndani yake. Wale simba walipomshambulia mama yake, alisimama na kupiga kelele, "Mimi pia ni Mkristo." Maafisa wa Kiroma wakamkamata na kumtupa kwa nguvu kwa wanyama wale wenye njaa.

Ufunuo
12:11 huonyesha picha ya kanisa linaloshinda ambalo limejaa washindi:
mitume, wafia dini, wanamatengenezo ya kanisa, na Wakristo wengineo
waaminifu. Upole, uaminifu, ujasiri, na ushindi wao umenguruma kushuka
katika karne nyingi na kuupindua ulimwengu.
Kwa
kuwa Shetani alishindwa kumwangamiza Yesu alipoishi hapa duniani, sasa
anajitahidi sana kumwangamiza Kristo anayeishi ndani ya kanisa lake.
"Joka
lilipotambua kwamba limetupwa chini duniani, likaanza kumwinda yule
mama aliyekuwa amejifungua mtoto wa kiume. Lakini mama huyo akapewa
mabawa mawili ya tai apate kuruka mbali sana na hilo joka, mpaka mahali
pake jangwani ambapo angehifadhiwa salama kwa muda wa miaka mitatu na
nusu. Basi, joka likatapika maji mengi kama mto, yakamfuata huyo mama
nyuma ili yamchukue. Lakini nchi ikamsaidia huyo mama: ikajifunua kama
mdomo na kuyamezaaa maji hayo yaliyotoka kinywani mwa hilo joka - (Ufunuo
12:13-16).

Akiwa
amekasirika vibaya sana dhidi ya kushindwa kwake pale msalabani, Shetani
akaielekeza ghadhabu yake dhidi ya Kanisa lile alilolianzisha Yesu.
Katika miongo [miaka kumi-kumi] iliyofuata baada ya kusulibiwa kwake
Kristo, maelfu waliuawa katika ule uwanja wa duara uliojengwa mjini
Roma (Colosseum), maeneo tupu ya pembe mraba yaliyokuwa mijini, magereza
yale ya chini ya ardhi, na katika maficho ya jangwani.
Mwanzoni
wale wenye mamlaka [serikali] ya kidunia walianzisha hayo mateso. Lakini
baada ya kufa wale mitume badiliko lilitokea taratibu ndani ya kanisa
lile. Katika kipindi kile cha karne ya pili, ya tatu, na ya nne, wengi
ndani ya kanisa lile walianza kuzibadili kidogo zile kweli zilizokuwa
zimefundishwa na Kristo pamoja na mitume wake. Viongozi fulani, walioasi
hata wakaanza kuwatesa Wakristo wale waliosisitiza kuwa na usafi wa
itikadi [imani] za Agano Jipya.
Wataalam
wa Biblia wanakadiria kwamba takriban milioni 50 ya wale waliokuwa waaminifu
waliuawa. Katika jitihada yake ya kulizamisha na kuliangamiza kanisa,
Ibilisi alitoa "mto" wa mateso ili kulifanya "lichukuliwe
[lile kanisa] na mkondo ule wa mto." "Lakini nchi ikamsaidia
yule mwanamke kwa… kuumeza ule mto" wa mateso na mafundisho
ya uongo.
Katika
kipindi cha mateso ya Zama za Kati [1100-1500], kanisa la kweli lilijiondoa
kutoka katika uongozi ule ulioasi na kujificha "Nyikani, mahali
alipoandaliwa na Mungu, ili wamlishe muda wa siku 1,260" (fungu
la 6). Utabiri huo ulitimizwa katika kipindi cha miaka 1260 ya mateso
kuanzia mwaka wa 538 hadi mwaka wa 1798 B.K. (siku moja mara nyingi
husimama badala ya mwaka mmoja katika unabii wa mifano wa Biblia, angalia
Ezekieli 4:6).
Katika
kipindi cha karne za giza Wakristo waaminifu walioiamini Biblia walipata
kimbilio lao po pote walipoweza kupapata kwa mfano, katika mabonde ya
Wawaldensia wa Italia magharibi na Ufaransa mashariki, na katika kanisa
la Kikeltiki [Waskoti Waairishi, Waweishi] la visiwa vya Uingereza.
4.
Kanisa La Mungu Katika Siku Hizi Zetu
Jambo
hilo linatufikisha katika siku hizi zetu - yaani, kwenye kanisa la kweli
la Kristo tangu mwaka wa 1798. Kama ambavyo ingeweza kutarajiwa, yule
joka bado amewakasirikia watu wa Mungu. Vita kuu isiyoonekana kwa macho
inaendelea. Kwa kweli, Shetani anafanya shambulio lake kubwa kabisa
dhidi ya kanisa hilo muda mfupi tu kabla ya kuja kwake Yesu.
"Ndipo
yule Joka [Ibilisi] akamkasirikia sana yule mwanamke [Kanisa la Mungu],
akaenda zake afanye vita dhidi ya wazao wake waliosalia - wale wanaozitii
amri za Mungu na kuwa na ushuhuda wa Yesu." - (Ufunuo 12:17).
Unabii
huu unalenga katika siku zetu hizi. Shetani amekasirika sana; anafanya
vita dhidi ya wazao wa mwanamke waliosalia" - yaani, dhidi ya watu
wa Mungu wa siku hizi. Angalia alama zao zinazowatambulisha:
(1)Waumini
hao wa siku za mwisho wanao "ushuhuda wa Yesu." Kwa uaminifu
wakiyang'ang'ania mafundisho safi ya Neno la Mungu, wanamshuhudia Yesu
kwa njia ya maisha yao yenye nguvu nyingi ya Kikristo.

(2)
Wakristo hao wa siku za mwisho ni watu wa unabii. Kuupokea ule "ushuhuda
wa Yesu Kristo" kulimwezesha Yohana kukiandika kitabu kile cha
Ufunuo (Ufunuo 1:1-3). Kundi hilo la mwisho la waumini linapokea karama
ile ile: yaani, ushuhuda wa moja kwa moja toka kwa Mungu kupitia kwa
mjumbe wa kibinadamu. Karama yao ya unabii inalenga juu ya ufunuo wa
Mungu kuhusu utume wao na mwisho wao.
(3)
Wakristo hao wa siku hizi za mwisho wanatambulikana pia kama "wale
wanaozitii Amri [kumi] za Mungu." Hawatetei tu ukamilifu wa hizo
Amri Kumi, bali wanazitii pia. Upendo wa Mugu ulio mioyoni mwao unawaletea
utii unaotolewa kwa moyo wa furaha (Warumi 5:5; 13:8-10).
Wakristo
hao wa siku hizi za mwisho wanakifuata kielelezo cha Kristo na cha kanisa
lile la kwanza kwa kuzitii amri [kumi] za Mungu. Jambo hilo linamkasirisha
vibaya sana yule Joka - yaani, yule Ibilisi. Naye anapigana vita dhidi
ya "wazao" wa mwanamke "waliosalia" kwa sababu wanatoa
ushuhuda kwamba upendo wao kwa Mungu unawafanya wafuasi wake hao kuwa
watii. Kama vile Kristo alivyoagiza, aliposema:
"Mkinipenda, mtazishika amri zangu" - Yohana 14:15.
"Mkinipenda, mtazishika amri zangu" - Yohana 14:15.
Maisha
ya Wakristo hao wa siku hizi za mwisho yanaonyesha kwamba uwezekano
upo wa kumpenda Mungu kwa mioyo yetu yote na kuwapenda wenzetu kama
sisi tunavyojipenda wenyewe. Kulingana na maneno ya Yesu, sifa hizo
za tabia, yaani, upendo kwa Mungu na upendo kwa watu, hufanya muhtasari
wa Amri kumi za Mungu (Mathayo 22:35-40).
Ya
nne katika hizo amri inatutaka sisi kuitunza Jumamosi, siku ya saba
ya juma, kama Sabato. Kwa kuwa upendo wao kwa Yesu umezitia ndani ya
mioyo yao amri zote kumi [Ebr. 8:10; Kut. 20:3-17; Yak. 2:10-12], basi,
Wakristo hao wa siku hizi za mwisho ni Wasabato.
Sabato
ndicho kiini cha ujumbe wa mwisho wa Mungu kwa watu wake katika kitabu
cha Ufunuo, sura ya 12 na 14:6-15. Nguvu zote za mbinguni zinajipanga
nyuma ya Wakristo hao wa siku hizi za mwisho walioelezwa katika sura
hizo. Mwokozi wao aliye hai ndiye rafiki yao daima, na Roho Mtakatifu
anafanya kazi yake "kuwafanya imara kwa nguvu katika utu wao wa
ndani." Ahadi yake ni ya hakika. WATAmshinda Shetani "kwa
damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao" (Ufunuo 12:11).
Je!
unataka kuwa mmoja wa Wakristo hao wa siku hizi za mwisho ambao "wanazitii
amri [kumi] za Mungu" tena wa"na ushuhuda wa Yesu"? Kwa
nini usikate shauri sasa hivi?
No comments:
Post a Comment