Kanisa ni muunganiko wa binadamu wanaomwabudu Mungu katika Roho na Kweli ulimwenguni kote.
Mara kwa mara Mungu ametoa ujumbe wa pekee kukidhi mahitaji ya vizazi tofauti mbalimbali: Ujumbe wa kumsaidia Adamu na Eva baada ya dhambi kuiharibu dunia yao walipojiona uchi, Ujumbe kwa ulimwengu uliokuwako kabla ya gharika ile kuu ya maji, Ujumbe kwa miji ya Sodoma na Gomora kabla ya kuangamizwa kwa moto, Ujumbe kwa Israel wakati Ashuru au Babeli ilipowatishia n.k. Yesu alikuja na ujumbe maalum kwa siku zetu.
Sura ya 12 na 14 ya Ufunuo hutoa muhtasari wa ujumbe wa Mungu wa pekee kwa ajili yetu leo. Tutauangalia ujumbe huo ili tuzingatie sifa zinazotufanya kuwa sehemu ya Kanisa la Kristo leo.
.Kanisa Lilianzishwa Na Yesu
Maisha na mafundisho ya Yesu yalianzisha umoja wa imani na ushirika wa karibu sana katika kanisa lile la mitume walilolianzisha.Mitume wale walikuwa na uhusiano wa karibu kabisa na Kristo yule aliyefufuka.Paulo alitoa picha ya kifungo hicho cha karibu sana na kukilinganisha na uhusiano wa ndoa;"Naliwaposea Mume mmoja,yaani Kristo,ili niwalete ninyi kwake mkiwa bikira safi" 2 wakoritho 11:2.
Kulingana na maneno ya Paulo, Kanisa la Kikristo ni mwanamke safi, ni bibi-arusi wa Kristo,ishara inayofaa kabisa kwa kanisa lake alipendalo.Katika Agano la kale mithali iyo hiyo inatumika kuielezea Israeli,yaani,wateule wa Mungu.Mungu aliwaambia Israeli: wewe kama bibi-arusi ulinipenda mimi'(Yeremia 2:2) "Mimi ni mume wenu"(Yeremia 3:14).
sehemu ya pili ya somo hili tutaangalia kitabu cha Ufunuo kinavyozungumza juu ya kanisa kama mwanamke.
No comments:
Post a Comment