"MJIFUNZE KWANGU"
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu.
Mathayo 11:29.
"Mjifunze kwangu," alisema yule Mwalimu wa Mbinguni, "kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo...." Yatupasa kujifunza kujikana nafsi, yatupasa kujifunza ujasiri, saburi, ushupavu, na upendo unaosamehe.... Iwapo tunayo imani ndani ya Yesu kama msaidizi wetu, iwapo macho yetu ya imani
yanaelekezwa kwake kila wakati, basi,tutakuwa kama Yesu katika tabia zetu. Atakaa ndani ya mioyo yetu, nasi tutakaa ndani yake Kristo. Tukiwa tumevikwa haki ya Kristo, maisha yetu yanafichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Atakuwa mshauri wetu. Tukimwomba kwa imani, atatufungua ufahamu wetu.... Mafundisho aliyotupa Kristo yatawekwa katika matendo.
Kristo, Kielelezo Chetu, anapowekwa daima mbele ya macho ya akili zetu, hapo ndipo tabia mpya zitaweza kukuzwa, mielekeo yetu mibaya yenye nguvu tuliyorithi pamoja na ile tuliyojizoeza wenyewe itaweza kudhibitiwa na kushindwa, kujisifu kwetu kutatupwa mavumbini, tabia mbaya za zamani za mawazo zitapingwa daima, kupenda kwetu makuu
kutajionyesha katika tabia yetu kwa dhahiri na kudharauliwa, nasi tutakushinda.
Kristo hana budi kuingia katika mawazo yetu yote, hisia zetu zote, na mapenzi yetu yote.
Anapaswa kutukuzwa katika mambo madogo sana ya utumishi wetu wa kila siku katika kazi ile aliyotupa kufanya. Wakati tunapoketi miguuni pake Yesu, badala ya kutegemea
ufahamu wetu wa kibinadamu au kufuata maneno ya hekima ya ulimwengu huu,tunapaswa kuyapokea maneno yake kwa shauku, tukijifunza kwake, na kusema, "Bwana,wataka mimi nifanye nini?" hapo ndipo hali yetu ya asili ya kujitegemea wenyewe, yaani,
kujitumainia wenyewe, kufuata mapenzi yetu wenyewe, itabadilika, na mahali pake itakuwapo roho ile ya kitoto, tiifu, inayokubali kufundishwa. Tunapokuwa na uhusiano sahihi na Mungu wetu, tutaitambua mamlaka ya Yesu katika kutuongoza sisi, na madai
yake kwetu kwamba tumpe utii usiokuwa na maswali.
Tutakuwa na mawazo ya hali ya juu kumhusu Yesu Kristo hata nafsi zetu zitajishusha chini. Mapenzi yetu yatakuwa ndani ya Yesu, mawazo yetu yatavutwa kwa nguvu kuelekea mbinguni. Kristo atakuwa hana budi kuzidi, wakati MIMI NINAPUNGUA....
Tutajizoeza kuwa na wema ule ulio ndani yake Kristo, ili sisi tupate kuakisi kwa wengine mfano wa tabia yake.
KUJITIA NIRA YA KRISTO
Kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi. Mathayo 11:30.
Kujitia nira ya Kristo, maana yake kufanya kazi kulingana na njia zake, kuwa mshirika mwenzi pamoja naye katika mateso yake na taabu zake kwa ajili ya wanadamu waliopotea.
Katika kuikubali nira yake Kristo ile ya kujizuia na utii, utaiona kwamba imekuwa msaada mkubwa sana kwako. Kujitia nira hii kunakuweka wewe karibu na ubavu wake
Kristo, naye anachukua sehemu ile iliyo nzito kuliko zote ya mzigo huo.
Nira na msalaba ni nembo zinazowakilisha jambo lile lile moja ----- kusalimisha mapenzi [nia] yetu yote kwa Mungu. Kujitia nira kunamwunganisha mwanadamu katika urafiki pamoja na yule mpendwa sana Mwana wa Mungu. Kuuinua msalaba juu
kunaiondoa nafsi moyoni, na kumweka mwanadamu mahali ambapo anajifunza kubeba mizigo yake Kristo. Hatuwezi kumfuata Kristo bila kujitia nira yake, yaani, bila kuuinua juu msalaba wetu, na kujitwika na kumfuata. Kama mapenzi yetu hayapatani na matakwa yale ya mbinguni, basi, inatupasa sisi kuyakataa matakwa yetu, kuachana na tamaa zetu tunazozipenda sana, na kukanyaga katika nyayo zake Kristo....
Wanadamu hujitengenezea nira ambazo huonekana kuwa ni nyepesi na za kupendeza kuvaa kwa ajili ya shingo zao wenyewe, lakini matokeo yake ni kwamba zinachubua vibaya mno. Kristo analiona jambo hilo, na kusema, "Jitie nira yangu. Nira ile unayoweza kuitia shingoni mwako, ukidhani inakufaa sana, haitakufaa hata kidogo. Jitie nira yangu, nawe ujifunze kwangu mafundisho ambayo ni ya muhimu kwako kujifunza."
Kazi yako sio kukusanya mizigo yako mwenyewe.... Mara nyingi sisi tunafikiri kwamba tuna wakati mgumu katika kuibeba mizigo yetu, na mara nyingi mno mambo yanakuwa hivyo, kwa sababu Mungu hajaweka mpango wo wote kwa ajili yetu kuibeba mizigo
hiyo; lakini tunapojitia nira yake na kuibeba mizigo yake, hapo ndipo tunaweza kushuhudia kwamba nira ya Kristo ni laini na mizigo yake ni myepesi, kwa sababu yeye ameweka mpango wa kuibeba hiyo [mizigo yake].
Hata hivyo, nira hiyo haitatupatia sisi maisha ya raha na uhuru na kujifurahisha nafsi zetu. Maisha yake Kristo yalikuwa ni maisha ya kujitoa mhanga na kujikana nafsi kwa kila hatua [aliyokwenda]; na kwa upendo unaodumu daima kama ule wa Kristo, mfuasi
wake wa kweli atatembea katika nyayo za Bwana wake; naye atakapokuwa anasonga mbele katika maisha haya, atazidi kujazwa na roho ile ile na maisha yale yale ya Kristo.
TUKIJIKANA NAFSI,NAFSI ZETU ZITAKUFA NA NAFSI YA KRISTO ITAISHI NDANI YETU.
Saturday, May 31, 2014
UJUE MOYO WAKO-sehemu ya tatu
NGUVU HALISI YA NIA
Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo. 2 Wakorintho 8:12.
Dini iliyo safi inahusika na matumizi ya nia. Nia ni uwezo unaotawala katika maumbile
ya mwanadamu, ikiuleta uwezo mwingine wote uliomo mwilini chini ya mamlaka yake.
Nia si kuonja wala mwelekeo, bali ni uwezo wa kuamua la kufanya ambao unafanya kazi
yake ndani ya wana wa wanadamu ama ukiwaelekeza kwenye utii kwa Mungu, ama kwenye uasi....
Bila shaka wewe unatamani kuyafanya maisha yako kuwa kama vile ambavyo yangefaa kukuwezesha kuingia mbinguni hatimaye. Mara nyingi unakata tamaa unapojiona mwenyewe kuwa u dhaifu katika uwezo wako wa kimaadili [tabia], unajikuta u mtumwa wa mashaka, tena umetawaliwa na tabia na desturi za maisha yako ya zamani ya dhambi.... Ahadi zako [maazimio yako] ni kama kamba zilizotengenezwa kwa mchanga....
Daima utakuwa hatarini mpaka hapo utakapoielewa nguvu halisi ya nia yako. Unaweza kuamini na kuahidi mambo yote, lakini ahadi zako au imani yako haina maana yo yote
mpaka hapo utakapoiweka nia yako nyuma ya imani yako na nyuma ya matendo yako.
Kama wewe unapiga vita ile ya imani kwa uwezo wako wote wa nia yako, utashinda.
Hisia zako, mvuto wako, mapenzi yako ya moyoni, mambo yote hayo hayaaminiki, kwa sababu hayawezi kutegemewa....
Lakini wewe huna haja ya kukata tamaa.... Ni juu yako mwenyewe kuisalimisha nia yako kwa nia ile ya Yesu Kristo; nawe unapofanya hivyo, Mungu atakushika mara moja na kufanya kazi yake ndani yako ili upate kutaka na kutenda yale yampendezayo Yeye.
Mwili wako wote ndipo utakuwa chini ya utawala wa Roho wake Kristo, na hata mawazo yako yatatawaliwa naye. Huwezi kuzitawala hisia zako, wala mapenzi yako ya moyoni, kama unavyotaka mwenyewe; lakini unaweza kuitawala nia yako [maamuzi yako], nawe kwa njia hiyo unaweza kufanya mabadiliko kamili katika maisha yako. Kwa kuisalimisha nia [mapenzi] yako kwa Yesu, maisha yako yatafichwa pamoja na Kristo katika Mungu na kuunganishwa na mamlaka ile ipitayo falme zote na mamlaka zote.
Utakuwa katika nguvu yake; na nuru mpya, yaani, nuru ile ya imani iliyo hai, itawezekana kwako kuwa nayo. Lakini nia yako ni lazima ishirikiane na nia yake Mungu....
Je! wewe hutasema, "Nitampa Yesu nia yangu, nami nitafanya hivyo sasa hivi," na kuanzia dakika hii hutakuwa upande wake Bwana kabisa?

Thursday, May 29, 2014
UJUE MOYO WAKO-sehemu ya pili
KUJIANDAA KWA SHULE ILE YA JUU ZAIDI
Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana wewe ndiwe Mungu wa wokovu
wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa. Zaburi 25:5.
Wale ambao ni wana wa Mungu hapa duniani wanaketi pamoja na Yesu katika Shule ya
Maandalizi, wakijitayarisha kupokewa katika Shule ile ya Juu Zaidi. Siku kwa siku
tunatakiwa kila mmoja kufanya maandalizi yake mwenyewe; maana katika majumba yale
ya kifalme kule juu hakuna ye yote atakayewakilishwa na mtu mwingine. Kila mmoja
wetu anapaswa kuusikia yeye mwenyewe mwito ule usemao, "Njoni kwangu,... nami
nitawapumzisha...."
Bwana Yesu amekulipia ada ya mafundisho. Yote yakupasayo kufanya ni kujifunza
kwake.
Upole kama ule wa Kristo utakaoonyeshwa kwa matendo katika Shule ile ya Juu
unatakiwa kuwekwa katika matendo na wakristo wote, wazee kwa vijana, katika Shule
hii ya Chini. Wale wote wanaojifunza katika shule hii ya Kristo wako chini ya mafunzo
wakiongozwa na wajumbe wale wa mbinguni [malaika]; wala haiwapasi kamwe kusahau
ya kwamba wao ni tamasha kwa ulimwengu huu, kwa malaika, na kwa wanadamu.
Wanapaswa kumwakilisha Kristo. Wanatakiwa kusaidiana wenyewe ili waweze kufaa
kuingia katika Shule ile ya Juu zaidi. Wanapaswa kusaidiana kila mmoja na mwenzake ili
wapate kuwa watakatifu na wenye utukufu, na kulizingatia sana wazo lile la kweli
linaloonyesha maana ya kuwa mtoto wa Mungu. Wanapaswa kusema maneno ya kutia
moyo. Wanapaswa kuiinua juu mikono iliyo dhaifu na kuyafanya imara magoti
yaliyolegea. Juu ya kila moyo panatakiwa kuandikwa maneno haya, kana kwamba ni kwa
kalamu yenye ncha ya almasi, "Hakuna kitu cho chote ninachokiogopa, isipokuwa tu
kwamba mimi sitaujua wajibu wangu, au nitashindwa kuutekeleza."...
Moyo uliodhibitiwa, maneno ya upendo na upole, humletea heshima Mwokozi wetu.
Wale wasemao maneno ya upole, maneno ya upendo, maneno yaletayo amani,
watatunukiwa vizuri sana.... Tunapaswa kumruhusu Roho wake kuangaza katika maisha
yetu ya nje ule upole na unyenyekevu wa moyo tuliojifunza kwake.
Yesu ndiye Mwalimu wetu Mkuu.... Anapenda sana, tena yu tayari sana kukuchukua
wewe katika ushirika wa karibu sana na Yeye mwenyewe. Yu tayari kukufundisha jinsi
ya kuomba kwa imani yenye matumaini na uhakika kama ile ya mtoto mdogo.
Jiandikishe upya jina lako kama mwanafunzi wa shule yake. Jifunze kuomba kwa imani.
Pokea maarifa yake Yesu.
Je! wewe huwezi kuketi miguuni pake Yesu na kujifunza kwake?
MUNGU ATUVUTE KWAKE TUJIFUNZE KWAKE KWANI YEYE NI MNYENYEKEVU WA MOYO.

UJUE MOYO WAKO...sehemu ya kwanza
KUJIFUNZA KATIKA SHULE YA KRISTO
Ni nani amchaye BWANA? Atamfundisha katika njia anayoichagua. Zaburi 25:12.
Yesu amefungua shule kwa ajili ya kuwaelimisha na kuwapa mazoezi wateule wake, nao wanapaswa kuendelea kujifunza daima kuyaweka katika matendo mafundisho yale anayowapa, ili wapate kumjua kabisa.
Wale wanaofikiri kwamba wao ni wema kiasi cha kutosha, wala hawafanyi kazi kwa bidii katika kuikamilisha tabia yao ya Kikristo, wataweka sanamu mioyoni mwao, nao wataendelea kutenda dhambi katika maisha yao mpaka dhambi kwao itaonekana kuwa si
dhambi tena....
Yesu anajitoa nafsi yake kwa kila mtu aliye mgonjwa, kwa kila mtu anayejitahidi kushinda. Roho Mtakatifu anamwombea kila mpiga mweleka mwaminifu, naye Kristo atayafanya maneno yake kuwa roho na uzima, yaani, kuwa uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila mtu aaminiye. Lakini wewe utashindwa kabisa utakapomruhusu yule mwovu kuutawala moyo wako, yaani, kuyaongoza mawazo yako.... Mungu hatadhihakiwa; hataukubali moyo uliogawanyika. Yeye anataka tumpe huduma yetu yote
kwa moyo wetu wote. Amelipa fedha ya fidia yetu kwa kujitoa nafsi yake mwenyewe kwa ajili ya kila mwana na binti ya Adamu....
Kristo anayo madai juu ya kila mtu; lakini wengi huchagua maisha ya dhambi. Wengine hawataki kuja kwa Yesu ili awape uzima. Wengine husema, "Naenda, Bwana," kwa
mwaliko wake, lakini hawaendi; hawajisalimishi nafsi zao kabisa ili kukaa ndani ya Yesu peke yake, ambamo ni uzima na amani na furaha isiyoneneka, yenye utukufu.... Je! hatutaamka na kuwa na hekima na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya umilele? tafuteni
neema yake Kristo kwa moyo wote, kwa uwezo wote, na kwa nguvu zote.
Mungu ametupa haki ya kumshikilia Yeye kwa njia ya maombi ya imani. Maombi yaliyojaa imani ndicho kiini cha dini safi, ni nguvu ya siri aliyo nayo kila Mkristo.
Tafuta muda wa kuomba, kuyachunguza Maandiko, kuiweka nafsi yako chini ya nidhamu ya Yesu Kristo. Uishi kwa kuwasiliana na Kristo aliye hai, na mara tu unapofanya hivyo, atakuchukua na kukushika kwa mkono wake ulio imara ambao hautakuachilia kamwe.
UBARIKIWE UNAPOFANYA MATENGENEZO KWA KUUJUA MOYO WAKO NA NEEMA YA BWANA WETU YESU KRISTO IWE NAWE DAIMA.

Wednesday, May 28, 2014
UNAWEZAJE KUMKANA KRISTO?
- Tunaweza kumkana kwa maneno yetu na kwa kusema mabaya juu ya wengine kwa mazungumzo ya upuzi, ubishi na maneno ya mzaha.
- Kwa maneno ya bure, yasiyo na maana au maneno makali ama kwa kusema uongo, kinyume cha kweli. kwa maneno yetu tunaweza kuonyesha kuwa kristo hayupo ndani yetu.
- Kwa tabia yetu tunaweza kumkana Kristo kwa kupenda raha ,kwa kuepuka kazi na mizigo ya maisha ambayo mtu mwingine hana budi kuichukua kama sisi tusipoichukua.
- Kwa kiburi cha nguo tuvaazo ,kwa kufuata mtindo wa ulimwengu au kwa mwenendo mbaya usio na adabu. 1Petro3:3-5.
- Kwa kupendelea maoni yetu wenyewe na kujaribu kuudumisha utu wa kale au kujihesabu wenyewe kuwa wenye haki.
Usalama tu kwa vijana ni kukesha kila wakati na kuomba kwa moyo mnyenyekevu. Kama twafanya hivyo malaika hutazama sala zetu, na ikiwa sala hizo hazijatoka katika midomo ya kusingizia wakati tukiwa katika hatari ya kufanya mabaya bila kujua na kutoa mvuto utakaowaongoza wengine kufanya mabaya, malaika atulindae atakuwa karibu nawe kukusaidia kutenda mema, akikuchagulia maneno, na kuongoza matendo yako.Zaburi 5:3-4 .
soma Mithal 3:3-4, 2Timotheo 2:19, Waebrania 12:14.
Tuesday, May 27, 2014
MBINU NA KANUNI ZA KUISHI NA WATU VIZURI
-Uwe na tabia ya kupenda watu kwa moyo wote. Mathayo 22:39
-Heshimu kila mtu na kila mtu umwone ni mtu muhimu. 1petro 2:17
-Usidharau mtu yeyote. mithali 13:1
-Usiwe msengenyaji na usiseme watu vibaya. 7:1-5
-Usipende kugombeza au kutukana watu. Tito 3:2
-Shukuru kwa kila jambo jema linapotendeka. 1Thesalonike 5:18
-Usiwe mtu mwenye kujipendekeza kwa watu. Mithali 29:5
-Uwe mnyenyekevu na usijivune kwa lolote lile, acha wengine wakusifu. 1petro 5:5
-Usiwe na kinyongo , fitina na usitunze chuki. mambo ya walawi 19:17-18
-Jipende na kujikubali kama ulivyo kimaumbile na uwezo wako, ndipo na watu watakupenda na kukubali kama ulivyo. mithali 19:8
-Usimharibie au kumchafulia mtu jina lake. walawi 19:16
-Usiwe na wivu juu ya mafankio ya wengine. yakobo 3:16
-Ukitaka watu wakuheshimu jiheshimu wewe kwanza. mathayo 7:12
-Usimcheke mtu mwenye shida, kasoro au anapokosea. 2wafalme 2:23
-Usiwe na tabia ya kukumbushakumbusha mtu makosa yaliyopita. mika7:19
-Kubali kikomo cha uwezo wa binadamu katika mambo fulani fulani na elewa kuwa hakuna aliye kamili kwa kila kitu. yakobo 3:2
KAMA UNATABIA FULANI MBAYA, MWOMBE MUNGU ATAKUSAIDIA NA KUJISAHIHISHA.

UZURI WA KITU UPO KATIKA MACHO YA MWONAJI
Watu wana mitazamo mbalimbali.
Macho ya Kristo pekee
hayachezi-chezi. Yanatulia yanapotazama. Zaidi ya tochi macho ya Yesu yanapenya
ngozi nakufika mpaka moyoni. Yanaona uzuri na udhaifu uliofichika. Mtazamo wa
Mungu ni sahii.
Hata kuhusu kanisa watu wanaliangalia tofauti
tofauti.
Kanisa linaweza kuonekana vizuri kwa macho ya mmoja ila kwa mwingine likaonekana vibaya. Tofauti ipo machoni, kwani uzuri wa kitu upo katika macho ya mwonaji:
Kwa mwingine kanisa ni mgodi wa hazina ya milele huku wengine
kanisa ni shimo lililojaa mapokeo ya zamani (uzuri wa kitu upo katika
macho ya mwonaji)
Kwa mwingine kanisa la
Lutherani ndio kanisa na huku kwa mwingine Katoliki ndio kanisa (uzuri wa kitu
upo katika macho ya mwonaji).
Tena kwa mwingine
kanisa ni Wapentekoste na kwa mwingine ni Wa Sabato (uzuri wa kitu upo katika
macho ya mwonaji).
Lakini macho yetu sio kiongozi amini. Leo yananionesha mwanamke
yule kuwa anapendeza. Kesho yananionesha mwingine na kunifanya nipoteze hamu na
wa jana. Hata kanisa nililoliona jana limejaa ngano leo naliona limejaa magugu
tupu. Macho yetu si kiongozi wa kuaminika, hayatulii.
TEMBELEA BLOG HII UPATE KUJIFUNZA MTAZAMO WA KRISTO JINSI ULIVYOFUNULIWA KATIKA BIBLIA ILI KWA NEEMA YA MUNGU UWEZE KUWA NA MTAZAMO KAMA WA YESU KRISTO.
Monday, May 26, 2014
MTU HUPIMWA KWA MAMBO MAKUU MATATU...!
NAMNA ANAVYO VAA: Mavazi ni moja ya kipimo cha nje kinachothihirisha falsafa na staha ya mvaaji. Kabla ujavaa vazi lako, jiulize kama vazi hilo ni la heshima, kikahaba n.k.
NAMNA ANAVYO ONGEA: Kwa kawaida mtu huongea yaliyo ujaza moyo wake, Hivyo tunavyozungumza kuna onyesha jinsi tulivyo.Kabla hujaongea jiulize Kama ingekuwa ni Yesu yuko katika mazingira yako angeweza kutamka maneno kama yako?
NAMNA ANAVYO KULA: Je ni mroho wa chakula au la! Inatupasa tujiulize kama tunadhamini chakula kuliko mambo ya kiroho au utu?
TUMTAZAME YESU KATIKA KILA JAMBO TUFANYALO NASI TUTAKUWA SALAMA KWANI YEYE PEKE YAKE NDIYE KIELELEZO CHETU KATIKA USAFI WA ROHO.

Sunday, May 25, 2014
KUWAITA VIJANA KUMCHA MUNGU
KUWAITA VIJANA WOTE!
Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana MUNGU, Tumaini langu tokea ujana wangu. Zaburi 71:5.
Yesu anamwita kila mpotevu, akisema, "Mwanangu, nipe moyo wako." Mithali 23:26....
Vijana hawawezi kuwa na furaha bila kuwa na upendo wa Yesu. Anangoja kwa huruma
kusikiliza maungamo ya wale walio watundu, na kuikubali toba yao. Anatazamia
kurudishiwa shukrani toka kwetu, kama vile mama anavyotazamia kuona tabasamu ya
kumtambua toka kwa mtoto wake ampendaye sana. Mungu aliye mkuu anatufundisha sisi
kumwita yeye Baba. Angependa sisi tuelewe jinsi moyo wake kwa dhati na kwa upole
unavyotupenda sana tunapokuwa katika maonjo na majaribu yetu....
Vijana wangekuwa wanaendelea daima kukua katika neema, na katika ujuzi wa ile
kweli. Muumbaji wa vitu vyote, ambaye hazina zote za hekima anazo, ameahidi kuwa
kiongozi wetu katika ujana wetu. Yeye aliyezishinda nguvu zote za uovu kwa ajili yetu
anatutaka tumsujudie. Hapawezi kuwapo na ujuzi wa juu kuliko ule wa kumjua Yeye
ambaye kumjua vema ni uzima na amani; hakuna upendo ulio safi na wenye kina kuliko
upendo ule wa Mwokozi wetu.
Kuna majaribu kila upande kuinasa miguu ya wale wasiojihadhari. Vijana wale
wasiomcha Mungu, wenye matendo mabaya wanao mvuto wenye nguvu kuwaongoza
wengine katika njia zile zilizokatazwa. Hao ni miongoni mwa vibaraka wa Shetani
wanaofanikiwa sana.... Mara nyingi wapenda dunia hii watakuja katika vazi la kirafiki, na
kujaribu kuingiza desturi na matendo yake. Hebu kila askari wa kweli awe tayari
kuvipinga vishawishi hivyo.
Shetani hutushambulia mahali pale tulipo na udhaifu; lakini hatuna haja ya kushindwa.
Shambulio hilo laweza kuwa kali na la muda mrefu, lakini Mungu ameahidi kutupatia
msaada wake, na kwa nguvu zake sisi tunaweza kushinda.... Kanuni na ahadi za neno la
Mungu zitatupatia silaha zenye uwezo wa Mungu kumpinga adui huyo.... Shetani
atachanganyikiwa na kushindwa anapokuta moyo wako
unajishughulisha na kweli ya Mungu. Pia mara kwa mara tunahitaji kuonekana kwenye
kiti kile cha neema. Maombi ya bidii na ya kudumu, yakiunganisha udhaifu wetu wa
kibinadamu na Uweza usio na kikomo wa Mungu, yatatupatia ushindi.
SOMA HABARI ZINAZOCHAPISHWA KATIKA BLOG HII UPATE NURU KUTOKA MBINGUNI

Friday, May 23, 2014
UZITO WA NENO "NAKUPENDA" ~VIJANA WA KILEO
UJUMBE MAALUM KWA VIJANA.
UZITO WA NENO "NAKUPENDA"
Katika mawazo na fikra nyingi za vijana wa kileo neno, "NAKUPENDA" linatumika vibaya sana bila kuzingatia muda, mahali na hata kiwango au hadhi ya mtu unayemuambia kuwa unampenda.
Neno hilo limekuwa kama salamu tu, bila shaka ni kama mtu anaposema shikamoo! limekuwa ni kigezo kikubwa cha kuwalaghai wasichana kisha kuwachezea na baadaye kuwaacha. Wasichana wengi nao wanapotamkiwa neno "NAKUPENDA" wanachanganyikiwa kabisa, linawavuruga kabisa mfumo wa fahamu na kuwanyima uwezo wa kufikiri tena juu ya maisha yao ya baadaye kwani wanajiona wao ndio wao, kitakachofuata baada ya hapo ni "NAKUPENDA PIA" na baadaye neno "NDIYO" katika kila jambo.
Sasa basi, kwa nini wewe kijana wa kiume uliyelelewa na kufunzwa adabu njema, umtamkie msichana kuwa UNAMPENDA wakati huna uhakika na hisia zako na humaanishi unachokisema? Kwa nini basi usitumie neno "NAKUPENDA" wakati wa ndoa yako utakapowadia? Au kwa nini neno hili lisitumike katika kujenga mahusiano ya kawaida tu?
Tafakari kwa makini, unatakiwa kuwa na uhakika wa hisia zako.
Kwa akina dada nao, kwa nini ukubali kudanganyika eti kwa vile mtu amekuambia anakupenda? Tuwe makini kutamka neno hili na tutafakari jinsi ya kulipokea.
TEMBELEA BLOG HII KILA SIKU UPATE HEKIMA KUTOKA JUU MBINGUNI.

ASOMAYE NA AFAHAMU
(ASOMAYE NA AFAHAMU) Mathayo 24:15
Kitabu cha Danieli kinahusu nyakati zetu hizi za mwisho.
Kuelewa mambo yaliyo mbele yetu ni muhimu sana, maana ama
tutapata uzima wa milele, ama mauti ya milele katika mkabala
wetu na matukio hayo yanayokuja. Hivyo si suala dogo kujifunza
unabii wa kitabu cha Danieli kwa wote wanaotaka uzima wa milele.
Yesu akizungumza na wanafunzi wake juu ya matukio ya siku za
mwisho alisema, "Basi hapo mtakapoliona Chukizo la Uharibifu,
lile lililonenwa na Danieli, limesimama mahali patakatifu
(asomaye na afahamu)". Mathayo 24:15. Hatari kubwa i mbele
yetu! Yesu anataka kila asomaye alifahamu Chukizo hilo la
Uharibifu linalokuja ili atakapoliona akimbie kuokoa maisha yake
(Mt. 24:16-22). Chukizo la Uharibifu limetajwa mahali patatu
katika kitabu cha Danieli (Dan. 9:26,27; 11:31; 12:11). Lina
majina mengi katika kitabu cha Danieli na cha Ufunuo ----- Pembe
Ndogo, Mnyama, na kadhalika. Utashangaa kujua kwamba "mnyama"
katika lugha ya taaluma ya unabii sio tusi wala kashfa kama
wengi wanavyodhani. Maana yake ni "mfalme au ufalme"
(Dan.7:17). Biblia inajitafsiri yenyewe!
Hivi maana ya "chukizo" ni nini? Soma 2 Wafalme 21:1-11 na
Kumbukumbu la Torati 18:9-14. Kumbe! Chukizo ni kuabudu
sanamu, kuwaomba wafu, kushughulika na mapepo, uchawi au
ushirikina, kuabudu jua na nyota za mbinguni, na kadhalika.
Mataifa, yaani, wapagani hufanya mambo hayo. Je! "uharibifu"
ni nini? Sio kuharibu vitu, bali ni kuwaangamiza, yaani, kuwaua
watu (Dan.8:24,25). Kwa hiyo, Chukizo la Uharibifu ni mamlaka
au utawala au ufalme unaoabudu sanamu, unaowaomba wafu, ulio na
ushirikina, na, zaidi ya hayo, unaowaangamiza "watakatifu",
yaani, "hao wazishikao Amri [Kumi] za Mungu na Imani ya Yesu
(Ufu.14:12; Kut. 20:3-17; Yak. 2:10-12). Paulo analiita "mtu
wa kuasi, mwana wa uharibifu [mwuaji], mpingamizi [au Mpinga
Kristo] (2 The. 2:3,4].
Bila kila mtu kumjua huyo, Yesu Kristo hawezi kuja duniani.
Tutaendelea kusumbuka na magonjwa, umaskini, na dhiki. Je! si
jambo la muhimu kabisa kuijua mamlaka hiyo ili kujua la kufanya
kuokoa maisha yetu, si yale ya kimwili, bali ya kiroho ili
tupate kuishi milele? (Mt. 10:26-33; Yoh.6:39-40; Ufu.12:11).
Kufa au kutokufa si hoja, bali kujiweka tayari kumlaki Yesu
Kristo atakapokuja juu ya mawingu ya mbinguni (Ufu. 2:10; Mt.
24:29-31).
Mpendwa Msomaji, je! kwa neema yake Mungu unataka kuwa
tayari kujiunga na watakatifu ulimwenguni kote? Soma Danieli,
na ufahamu. Kabla hujaanza kusoma somo, omba ili Mungu akupe
Roho wake atakayekufundisha kweli yote (Yohana 16:13-15). Mungu
na akubariki!
ENDELEA KUTEMBELEA BLOG HII KILA SIKU UJUE MANENO YA UNABII

JE AGANO LA KALE LINA HABARI ZA YESU?
SWALI:
NI NANI ALIYEFUNULIWA KATIKA MAANDIKO MATAKATIFU YOTE?
JIBU:
YESU KRISTO,
"Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake;na hayo ndiyo yanayonishuhudia" Yoh.5:39.
Biblia nzima ni ufunuo wa kazi ya Kristo, hasa wa kazi yake ulimwenguni kwa ajili ya wanadamu. Kristo aliwafundisha wanafunzi wake juu yake mwenyewe kwa Maandiko ya Agano la Kale."Akaanza kutoka Musa na manabii wote,akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe" Luka 24:27.
FAHAMU KWAMBA:
YESU KRISTO WA NAZARETH NDIYE NJIA,KWELI NA UZIMA.YEYOTE AJAE KWAKE ATAPATA MAJI YA UZIMA BURE.
IJUE KWELI NAYO KWELI ITAKUWEKA HURU! BIBLIA YOTE KUANZIA KITABU CHA MWANZO HADI KITABU CHA UFUNUO NI NENO LA KRISTO NA NENO LAKE NDIYO KWELI.
SWALI:
Mwalimu mwema nifanye nini ili ni uridhi UFALME WA MUNGU?
JIBU:
Yesu akajibu, Je,wazijua AMRI?Soma Kutoka 20:1-17(AMRI KUMI ZA MUNGU). Kijana akajibu Hizo nimezishika toka utoto wangu.
Yesu akampenda akamwambia Kauze mali zako uwape maskini kisha unifuate.
FAHAMU KWAMBA:
INATUPASA KUZISHIKA AMRI ZA MUNGU NA KUMFUATA KRISTO ILI TUWEZE KU URIDHI UFALME WA MUNGU (ku upata uzima wa milele)
TAFUTENI KWANZA UFALME WA MUNGU NA HAKI YAKE NA MENGINE MTAZIDISHIWA.
TEMBELEA BLOG HII KILA SIKU UJIFUNZE MAMBO MUHIMU ILI UWEZE KUPATA UZIMA WA MILELE
"Basi, enendeni,kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi,.. mkiwafundisha kushika yote niliyowaamuru ninyi: na tazama,mimi nipo pamoja nanyi siku zote,hata mwisho wa dunia" Alisema Bwana wetu.

Thursday, May 22, 2014
THE DEEPEST AND MOST LASTING HAPPINESS
SECRET OF HAPPINESS AND EVERLASTING LIFE.
We often fall into the trap of thinking a new car, job promotion, beauty makeover, or some level of fame will make us happy. And often they do—for a time. But it never lasts because wealth, power, beauty and fame simply don’t bring lasting happiness, as much as we wish they would. Rather, true happiness comes from following Christ’s example and developing Godlike attributes such as goodness, love, justice and mercy. It comes from serving others and helping them to follow the example and teachings of Jesus Christ. It comes from overcoming the appetites of our human bodies and instead following the promptings of the Spirit. It comes from working hard and having a healthy lifestyle, friends, family, and personal achievements. Regardless of what you do or don’t have in this life, your deepest, most lasting happiness will come from knowing God’s will and do the will of God.
VISIT THIS BLOG EVERY DAY TO LEARN THE WILL OF GOD AS REVEALED TO US THROUGH HIS ONLY BEGOTTEN SON JESUS CHRIST (THE MESSIAH).

UMEWAHI KUTEMBEA KATIKA GIZA NENE BILA TAA?
Karibuni, kwenye blog ambayo itakuwa ikiongelea Neno la Uzima wa Milele.
Tafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na Haki yake na Mengine Mtazidishiwa.
Je, umewahi kutembea katika giza nene bila kuwa na taa?
mara nyingi mtu anapotembea kwenye giza nene anaweza kujikwaa,kuanguka,kuumia,au hata kupotea njia.
ili tuweze kuona kwa macho yetu, ni lazima tuwe na mwanga(taa).Jambo hilo linaendana kabisa na mambo ya kiroho.Maana ili tuweze kuona kwa macho yetu ya Kiroho,ni lazima tuwe na taa.Mungu ametupatia taa ya kutumulikia katika ulimwengu huu wa giza nene ambamo watu wengi hupotea njia. TAA HIYO NI BIBLIA.
Katika Zaburi 119:105 Daudi anasema, "Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu."
Biblia siyo macho bali ni taa yetu. Kama taa ni ya maana katika giza,ni lazima tuitumie.Haitatusaidia kama tukiiacha ndani ya nyumba bila kuiwasha. Hivyo kama Biblia ni taa yako katika dunia hii ya giza,ni lazima uisome. Unapaswa kuyajua maneno na mafundisho yake
Mafarisayo walikuwa vipofu kwa sababu walikuwa na mapokeo na mawazo yao wenyewe kiasi kwamba hawakuwa na hamu sana ya kuichunguza Biblia. Yesu alijua kwamba walikuwa wanakosea sana, hivyo aliwaonya, aliwaambia, "Msidhani kwamba mimi nitawashitaki, yuko anayewashitaki,ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi, kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu. Lakini msipoyaamini maandiko yake mtayaamini wapi maneno yangu?" YOHANA 5:45-47.
Kwa wale ambao walikuwa wanakaidi maneno ya Musa na Manabii, Yesu aliwaambia, "Wasipowasikia Musa na Manabii, hawatashawishiwa hata mtu akifufuka katika wafu." LUKA 16:31.
FUATILIA BLOG HII UPATE MAFUNDISHO YA KWELI YOTE ILIVYO FUNULIWA KATIKA BIBLIA .

Subscribe to:
Posts (Atom)