-Uwe na tabia ya kupenda watu kwa moyo wote. Mathayo 22:39
-Heshimu kila mtu na kila mtu umwone ni mtu muhimu. 1petro 2:17
-Usidharau mtu yeyote. mithali 13:1
-Usiwe msengenyaji na usiseme watu vibaya. 7:1-5
-Usipende kugombeza au kutukana watu. Tito 3:2
-Shukuru kwa kila jambo jema linapotendeka. 1Thesalonike 5:18
-Usiwe mtu mwenye kujipendekeza kwa watu. Mithali 29:5
-Uwe mnyenyekevu na usijivune kwa lolote lile, acha wengine wakusifu. 1petro 5:5
-Usiwe na kinyongo , fitina na usitunze chuki. mambo ya walawi 19:17-18
-Jipende na kujikubali kama ulivyo kimaumbile na uwezo wako, ndipo na watu watakupenda na kukubali kama ulivyo. mithali 19:8
-Usimharibie au kumchafulia mtu jina lake. walawi 19:16
-Usiwe na wivu juu ya mafankio ya wengine. yakobo 3:16
-Ukitaka watu wakuheshimu jiheshimu wewe kwanza. mathayo 7:12
-Usimcheke mtu mwenye shida, kasoro au anapokosea. 2wafalme 2:23
-Usiwe na tabia ya kukumbushakumbusha mtu makosa yaliyopita. mika7:19
-Kubali kikomo cha uwezo wa binadamu katika mambo fulani fulani na elewa kuwa hakuna aliye kamili kwa kila kitu. yakobo 3:2
KAMA UNATABIA FULANI MBAYA, MWOMBE MUNGU ATAKUSAIDIA NA KUJISAHIHISHA.
nitafanyaje nisiwe na kinyongo na nisituze hasira moyoni mwangu mtu akiniuzi?
ReplyDelete1.Jifunze kusamehe makosa ya watu. Mathayo 18:21-22
Delete2.Heshimu na kuvumilia mawazo na maoni ya wengine ambayo nitofauti na yako. Mithali 12:15
3.Usitawaliwe na misisimko au jaziba. Mithali 14:29
4.usilipize kisasi. Warumi 12:19-20
5.usiwe na msimamo mkali kupita kiasi. Mhubiri 7:16, 2Timoth 4:5