Thursday, May 22, 2014

UMEWAHI KUTEMBEA KATIKA GIZA NENE BILA TAA?

Karibuni, kwenye blog ambayo itakuwa ikiongelea Neno la Uzima wa Milele.

Tafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na Haki yake na Mengine Mtazidishiwa.

Je, umewahi kutembea katika giza nene bila kuwa na taa?
mara nyingi mtu anapotembea kwenye giza nene anaweza kujikwaa,kuanguka,kuumia,au hata kupotea njia.
ili tuweze kuona kwa macho yetu, ni lazima tuwe na mwanga(taa).Jambo hilo linaendana kabisa na mambo ya kiroho.Maana ili tuweze kuona kwa macho yetu ya Kiroho,ni lazima tuwe na taa.Mungu ametupatia taa ya kutumulikia katika ulimwengu huu wa giza nene ambamo watu wengi hupotea njia. TAA HIYO NI BIBLIA.
 Katika Zaburi 119:105 Daudi anasema, "Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu."

Biblia siyo macho bali ni taa yetu. Kama taa ni ya maana katika giza,ni lazima tuitumie.Haitatusaidia kama tukiiacha ndani ya nyumba bila kuiwasha. Hivyo kama Biblia ni taa yako katika dunia hii ya giza,ni lazima uisome. Unapaswa kuyajua maneno na mafundisho yake

Mafarisayo walikuwa vipofu kwa sababu walikuwa na mapokeo na mawazo yao wenyewe kiasi kwamba hawakuwa na hamu sana ya kuichunguza Biblia. Yesu alijua kwamba walikuwa wanakosea sana, hivyo aliwaonya, aliwaambia, "Msidhani kwamba mimi nitawashitaki, yuko anayewashitaki,ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi, kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu. Lakini msipoyaamini maandiko yake mtayaamini wapi maneno yangu?" YOHANA 5:45-47.

Kwa wale ambao walikuwa wanakaidi maneno ya Musa na Manabii, Yesu aliwaambia, "Wasipowasikia Musa na Manabii, hawatashawishiwa hata mtu akifufuka katika wafu." LUKA 16:31.

FUATILIA BLOG HII UPATE MAFUNDISHO YA KWELI YOTE ILIVYO FUNULIWA KATIKA BIBLIA .

1 comment: