Hata kuhusu kanisa watu wanaliangalia tofauti
tofauti.
Kanisa linaweza kuonekana vizuri kwa macho ya mmoja ila kwa mwingine likaonekana vibaya. Tofauti ipo machoni, kwani uzuri wa kitu upo katika macho ya mwonaji:
Kwa mwingine kanisa ni mgodi wa hazina ya milele huku wengine
kanisa ni shimo lililojaa mapokeo ya zamani (uzuri wa kitu upo katika
macho ya mwonaji)
Kwa mwingine kanisa la
Lutherani ndio kanisa na huku kwa mwingine Katoliki ndio kanisa (uzuri wa kitu
upo katika macho ya mwonaji).
Tena kwa mwingine
kanisa ni Wapentekoste na kwa mwingine ni Wa Sabato (uzuri wa kitu upo katika
macho ya mwonaji).
Lakini macho yetu sio kiongozi amini. Leo yananionesha mwanamke
yule kuwa anapendeza. Kesho yananionesha mwingine na kunifanya nipoteze hamu na
wa jana. Hata kanisa nililoliona jana limejaa ngano leo naliona limejaa magugu
tupu. Macho yetu si kiongozi wa kuaminika, hayatulii.
TEMBELEA BLOG HII UPATE KUJIFUNZA MTAZAMO WA KRISTO JINSI ULIVYOFUNULIWA KATIKA BIBLIA ILI KWA NEEMA YA MUNGU UWEZE KUWA NA MTAZAMO KAMA WA YESU KRISTO.
kweli kabisa tuombe Mungu atupe macho ya ndani ambayo yatatusaidia kuona kama aonavyo Mungu
ReplyDeleteAmina Ledina. Yesu ametupatia Roho Mtakatifu anayeshuhudia ndani yetu na kutuweka katika kweli yote tukiamini uongozi wake katika maandiko Petro wa pili 1:21
Deleteamen
ReplyDeleteHakika uzuri wa kitu upo katika macho ya mtu, lakini kuyatazama yale yaliyo bora na salama katika maisha yetu, hatuna budi kuomba Roho Mtakatifu awe kiongozi na dira katika maisha yetu ili tupate macho ya rohoni amabayo hayata babaika na vizuri vya duniani bali yatatazama yale ya kumpendeza Mungu.
ReplyDelete