Friday, October 10, 2014

JINSI YA KUOKOLEWA -Sehemu ya pili

 Wokovu ni Zawadi Kutoka kwa Mungu

Upendo wa Kweli hujulikana kwa matendo yake. wakati mwingine kama binadamu tunaweza kusema tunampenda mtu fulani , wakati matendo yetu yanadhihirisha kinyume chake.(Yohana 3:17,18). Hilo kwa Mungu haliwezi kutokea. Upendo wake unaakisiwa katika matendo yake. kutokana na upendo, alimtoa Mwana wake wa pekee kwa ajili ya wokovu wetu. Kwa kufanya hivyo, Mungu alitupatia vyote alivyo navyo, ambavyo ni Yeye mwenyewe.
Upendo wa Mungu haubagui, au hata kutegemea matendo yetu. Mungu anaupenda ulimwengu, huku ni kusema, binadamu wote, pamoja na wale wasiompenda.

Soma Luka 18:9-14. Huenda tumeusoma mfano huu lakini hatushangazwi na hukumu ya Yesu:"Nawa ambia, huyu (mtoza ushuru) alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule" (luka 18:14) . Hata hivyo , wale waliomsikia Yesu akitamka hukumu hii lazima walishangazwa. Je, haya hayakuwa matokeo yasiyo ya haki? Ndiyo, hakustahili kabisa. Hivi ndivyo wokovu ulivyo. Ni zawadi kutoka kwa Mungu.Zawadi hazifanyiwi kazi ila tu huwa zinapokelewa/zinakubaliwa. Hatuwezi kununua wokovu; tunaweza tu kuupokea. Ingawa Yesu alitumia neno Neema kwa nadra, lakini alifundisha waziwazi kwamba wokovu ni kwa njia ya Neema, na Neema ni kupewa kile usichostahili. 

Tumwombe Mungu atuwezeshe kuipokea zawadi ya wokovu kama Mtoza Ushuru na Tusi ikatae kwa kudhani ni haki yetu kama mfarisayo alivyofanya. Sote tumetenda dhambi na kuhitaji zawadi ya wokovu. Hakuna hata mmoja anayeweza kujiokoa mwenyewe tangu Adamu alipo tenda dhambi kwani sote tulitumbukia shimoni na kumhitaji Mwokozi ambaye hajawahi kutenda dhambi yaani Kristo peke yake.
akiisha kutukomboa kutoka katika shimo la dhambi Kristo anatualika kuishi maisha ya utakatifu kama Yeye mwenyewe alivyoishi kwa kuzishika Amri za Mungu hivyo kuyafanya mapenzi ya Baba yake siku zote na Kukaa katika Pendo la Baba wa Mbinguni.

usikose sehemu ya tatu ya somo hili ujifunze maarifa kamili ya wokovu.

Wednesday, October 8, 2014

JINSI YA KUOKOLEWA-Sehemu ya kwanza

"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele" (Yohana 3:16)

"Kifo" huwa tunasema, 'ni sehemu tu ya maisha." Hapana, Kifo ni kinyume cha maisha, siyo sehemu yake. Lakini kwa kuwa tumekizoea sana kifo tunaona hivyo kinyume na uhalisi wake. vyovyote tutakavyo elewa ,
jambo moja ni la hakika: Bila msaada wa Mungu, Kifo cha milele kingekuwa ndio mwisho wetu wote.

Kwa bahati nzuri, msaada huo umekuja. Mungu katika upendo wake usio na ukomo, anatupatia wokovu kwa njia ya Kristo. wakati malaika alipotangaza kuzaliwa kwa masihi, alimwita YESU ambalo ni neno la kiebrania lenye maana ya Wokovu. maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao (Mathayo 1:21)
katika somo hili la jinsi ya kuokolewa tutatafakari kazi ya Yesu ya kuokoa. Tutajielekeza katika msingi wa wokovu wetu na baadaye katika matokeo yake.
Biblia iko wazi. Tuna uchaguzi  wa aina mbili tu kuhusu dhambi zetu,

1. Tunakubali malipo ya Kristo kwa ajili ya dhambi zetu katika msalaba wa Kalvari, AU
2. Tunazilipia dhambi zetu kwenye ziwa la moto katika mauti ya pili

Kwa wanaokubali kumwamini Kristo kwa kushika Amri za Mungu na Imani ya kristo (ufunuo 12:17) mauti ya pili haina nguvu. Kadiri tunavyopitia tena zawadi ya neema ya Mungu kwa njia ya Kristo, hebu kwa unyenyekevu tuifanye upya tena Imani yetu kwa Yesu kama Mwokozi wetu binafsi.

Endelea kutembelea katika sehemu ya pili ya somo hili upate ufunguo wa maarifa ya maisha ya wokovu.
UBARIKIWE NA BWANA.

Friday, September 19, 2014

KUKAA KWA AMANI NA MWAJIRI

Mungu hupenda watu wa aminifu kwa  wa ajiri wao. Kama ume ajiriwa unapaswa kuzingatia yafuatayo:

1. Ukiwa kazini tumia muda vizuri. Siyo vizuri kutumia muda mwingi kwa simu,maongezi na marafiki au kwa matembezitembezi ndani ya masaa ya kazi. Hakikisha unafanya kazi kwa manufaa ya mwajiri/kampuni katika masaa yako ya kazi kwa mujibu wa mkataba wako wa kazi.

2.Siyo tabia nzuri kutumia mali ya mwajiri vibaya kama vile, umeme N.K kwa matumizi binafsi, marafiki au jamaa zako. Dhamini mali ya mwajiri kama unavyo dhamini mali yako mwenyewe kwani huwezi kufurahia kutapanya mali yako ovyo ovyo.Kumbuka mwajiri anatoa gharama kununua hizo mali kwa manufaa ya kampuni kama unavyo gharimia mali za nyumbani kwako kwa manufaa ya familia yako.

3. Usifanye mahali pa kazi ni mahali pa kukutania na marafiki kwa maongezi yenu binafsi.

4. Ukiwa kiongozi usitumie madaraka yako uliyopewa kuwagandamiza au kuwanyanyasa wengine hata kuwalazimisha kufanya maovu, kama vile mapenzi au kuwatumia kufanya mambo yako binafsi kwa uonevu.

Tumwombe Mungu atuwezeshe kuwa wa aminifu kwa kila jambo.

Tuesday, September 9, 2014

KUTOKA MAUTI HADI UZIMA WA MILELE

YESU KRISTO alikuja ili kila amwaminiye asipotee ila awe na uzima wa milele.

 Jambo lililomleta Mwana wa Mungu duniani ni Kumkomboa mwanadamu aliyetenda dhambi kutoka katika dhambi zake na kufanywa mwana wa Mungu na kuwa mtakatifu kama baba wa mbinguni alivyo.

Roho mtakatifu anamwezesha aliye amini kuishinda dhambi.  Tumruhusu roho wa kweli atuongoze kwa kwenda kwa roho ili tusizitimize tamaa za mwili kwani mwili hutamani kushindana na roho ila tuki ufuata mwili tutabaki mautini hivyo imempasa kila anayeitwa kwa jina la Kristo kuenenda kama yeye alivyo enenda alipokuwa hapa duniani na kutuachia kielelezo.

Endelea kutembelea hapa tujifunze mapenzi ya Baba wa Mbinguni ili tuweze kuyafanya kwani watakao karibishwa mbinguni siku ya mwisho si wale wanaosema Bwana Bwana ila wanao yafanya mapenzi ya Mungu.

YESU KRISTO NI LANGO PEKEE LA KUINGILIA MBINGUNI

MSIPO INYWA DAMU YANGU NA KUULA MWILI WANGU HAMTAWEZA KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU.
Maneno hayo ni roho na walio wa rohoni watayatekeleza kiroho.

*Maana ya kunywa Damu ya Yesu Kristo kiroho:
Ndani ya Damu ndimo mlimo UHAI. Sote tumefanya dhambi na kustahili mauti kwani mshahara wa Dhambi ni mauti, ila Karama ya MUNGU ni UZIMA WA MILELE ULIO KATIKA KRISTO YESU.Tunapo mkiri Yesu Kuwa MWOKOZI WA MAISHA YETU KWA KUTUBU DHAMBI ZETU NA KUREJEA KWA KUJISALIMISHA NIA ZETU KWA NIA YA KRISTO INAYOTII DAIMA MAPENZI YA MUNGU KATIKA HALI ZOTE; Tunakubali kafara yake Msalabani kama fidia ya dhambi zetu na hapo hapo  kifo cha Yesu msalabani huwa badala ya dhambi zetu na Sisi kuhesabiwa haki ya KRISTO KANA KWAMBA HATUJAWAHI KUTENDA DHAMBI HIVYO KUSTAHILI UZIMA WA MILELE.
TUNACHUKUA ROHO YA KRISTO. Ee MUNGU UTUPE ROHO YA KRISTO KWA WINGI MAISHANI MWETU.

*Maana ya kula mwili wa kristo kiroho:
Kristo ni NENO hivyo tukijazwa na Neno la Mungu nafsini mwetu na kuli ishi, Tuna ushiriki mwili mtukufu wa Kristo unaoweza kushinda MAJARIBU na Dhambi. Yesu ali ishi kwa kupitia Majaribu kama sisi lakini hakutenda dhambi hivyo kwa neema yake kama tutajikana nafsi na kumfuata tutaishinda dhambi na kuishi maisha matakatifu kama YEYE Alivyo ishi alipokuwa hapa Duniani. Tunapo mkiri Yesu Kuwa BWANA WA MAISHA YETU KWA KUISHI KWA KILA NENO LITOKALO KINYWANI MWA BWANA Ndipo Maisha ya Yesu yanakuwa kielelezo kwetu wakristo.UKIITWA  MKRISTO SHARTI UISHI MAISHA MATAKATIFU KAMA KRISTO. Ee MUNGU TUWEZESHE KUJAZWA NENO LAKO NA KULI ISHI ILI TUKAE KATIKA PENDO LAKO KAMA KRISTO BWANA WETU. AMINA.

YATUPASA KUZIACHA NJIA ZETU NA KUFUATA KILA NJIA INAYOELEKEZWA NA NENO LA MUNGU ILI TUPATE KUISHI.


 

Sunday, June 22, 2014

YESU ANAVYOLITAZAMA KANISA LAKE-sehemu ya tatu

Kanisa ni kama Jeshi lililoko uwanja wa vita
Math 16:18. Yesu anasema, “milango ya kuzimu haitalishinda [kanisa langu]” Kwa maneno hayo Yesu analiona kanisa kama Jeshi lililoko vitani linapambana. 

Lakini kanisa linashindana na nani? Linashindana na milango ya kuzimu. Na hapa kuzimu haiwakilishi kitu kingine isipokuwa mauti na kifo (uf 1:18). Kutoka kwa dhambi ya Adamu na wengine tunajua dhambi huzaa mauti (Yak 1:15). Na kama dhambi huzaa mauti, basi kanisa linapambana na dhambi na mauti--baba na mtoto. Adui wa kanisa sio wewe sio mimi na wala si wao; adui wa kanisa sio waislamu wala wapagani, adui wa kanisa sio viongozi wake wala washiriki wake; adui wa mtu sio baba yake, sio mme wake na wala sio watoto wake; labda tu kama wamegeuka kuwa mawakala wa kifo na mauti.

Kanisa halijatulia na haliwezi kutulia, mpaka limeondolewa uwanjani mwa vita, na dhambi na kifo vimetupwa Jehanamu. Wale wanaolilia utulivu na amani watusubiri malangoni mwa Yerusalemu. Huko ndiko hakuna maombolezo wala kilio wala maumivu (ufu 21:4). Wale wanalalamikia magugu yamezidi kutubanaa, uovu umetusonga zaidi, watusubirie siku ya hukumu ambapo wema na wabaya watatenganishwa milele. Kanisa ni Jeshi lililoko vitani, hivyo ndivyo Yesu anavyoliona.

Wewe na mimi tuko vitani. Inawezekana tumemkimbia Yesu, tumemkana hadharani,…. Hilo halitukatishi tamaa, tunajua tuko vitani. Tunaweza kutetereka na kujeruhiwa. Si neno, lakini hatutaitupilia mbali imani yetu. Mapambano yanaweza kuwa makali na majeraha yetu yakatupunguzia damu nyingi na kutuliza usiku kucha, lakini hatutatupilia mbali silaha yetu na imani yetu. Vidole vya wanao tushtumu na kutushtaki vinaweza kuelekezwa mioyoni mwetu na kutukumbusha tulivyomkana Yesu, hatutakata tamaa kutumaini wema wa Yesu. Kama tutabakia uwanja wa vita, hakika tutashinda. Maana Yesu anasema, “milango ya kuzimu”hayatamshinda muumini anayemtumainia Yesu kama Petro. Kama jiwe lililowekwa mlangoni mwa kaburi la Yesu halikuweza kumzuia Yesu siku ya Jumapili ile, kadhalika hata sisi “milango ya kuzimu haitatushinda” tunaposhikilia imani yetu. 

Kujua kuwa kanisa liko vitani kunanifanya nisilikatie tamaa ninapolitazama. Hata mimi kujua niko vitani kunanifanya nisijikatie tamaa katika mapambano ya maisha na imani. Kanisa ni la wapiganaji.


Mbele ya Yesu Kanisa ni zaidi ya jengo lilosimama mwambani, isipokuwa ni  Jeshi linaloshindana vitani. Hivyo ndivyo Yesu anataka kila mmoja alitambue kanisa lake hivyo. Na zaidi ya hapo Yesu analitambua kanisa kama mlinzi wa malango ya ufalme wa mbinguni

Friday, June 13, 2014

YESU ANAVYOLITAZAMA KANISA LAKE-sehemu ya pili

Kanisa(waumini wanaokiri Imani ya Petro kwa Yesu) wamepewa funguo za ufalme wa mbinguni.
angalia nami mathayo 16:19: “Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni”. Kwa maneno mengine Yesu anasema, "Kefa nitakupa  wewe funguo [wewe kefa ambaye hukutetereka kunikiri mimi kama Masihi na Mwana wa Mungu]. Wewe ni mshika funguo, mlinzi katika malango ya ufalme.” Unaweza kufunga na kufungua, kuruhusu na kuzuia, wewe ni mlinzi. 
Lakini Kefa au waumini wanaokiri imani ya Kefa ni walinzi wa namna gani mlangoni pa ufalme?  

Kabla hatujaelewa maana ya ufunguo: unakumbuka maneno ya Yesu kwa walimu wa dini katika Luka 11:52? Yesu alisema, “Ole wenu, enyi wana-sheria, kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.” Mahali pengine Yesu anawalaumu Mafarisayo (washika dini) kwa kosa hilo hilo (Math 23:13). Mara zote hizo funguo zinasimama badala ya maarifa na ujuzi waliopewa. Wana-sheria na Mafarisayo walikuwa na ujuzi wa maandiko ambao ungeweza kuwanufaisha wao na wengine. Lakini hawakutumia maarifa hayo ipasavyo.

Na kwa Petro na waumini wote, ujuzi na maarifa ya ufalme umetolewa.
Petro na waumini tumefunuliwa na Baba wa mbinguni kumwona Yesu kama Masihi na Mwana wa Mungu. Ufunuo huo ni ufunguo langoni mwa ufalme. Injili ya Yesu yaweza kuwafungulia malango ya ufalme wote wanaoipokea na kuwafungia malango hayo hayo wanapoikataa. Petro na sisi wakristo tumepewa funguo nyeti. 

Lakini mwenzetu Petro alizitumiaje funguo zake? Historia takatifu imerekodi kwa ufasaha jinsi mtume Petro alivyotumia maarifa ya kumjua Yesu masihi, kwa mfano: 
·   Petro alizitumia funguo hizo siku ya Pentekoste alipowaonesha wayahudi  kuwa Yesu ni Masihi na Mwana wa Mungu aliye hai. Akawaambia, “Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi” (Mdo 2:38). Na siku ile wengi kwa kumsikia Petro na kukubali  ujumbe wake walifunguliwa malango ya ufalme—tunaambiwa maelfu.
·  Mara nyingine Petro alimfungulia malango ya ufalme Kornelio na nyumba yake na wote wakaingia (Mdo 10)
· Mara nyingine Petro  akiwa na Yohana alimfungulia kiwete langoni mwa hekalu naye akapokea uponyaji
·  Mara nyingine Petro na Yohana wakawafungulia wasamaria nao wakapokea Roho Mtakatifu
·Lakini mara nyingine Petro alimfungia Anania na Safira na hawakuingia katika ufalme

Funguo alizopewa Petro ndizo tulizopewa. Tumepewa kuwafungulia watu wamjue Yesu kama Mkombozi nao wafunguliwe. Na kama kila mmoja wetu aliyepewa funguo hizi atazitumia wangapi wangepokea msamaha wa dhambi, wangapi wangefunguliwa na utumwa wa dhambi, wangapi wangepokea uponyaji. Yesu analitambulisha Kanisa kama walinzi katika malango ya ufalme. Ni bahati kuu kiasi gani lakini ni wajibu mzito namna gani kumiliki funguo za lango kuu la uzima?



Thursday, June 12, 2014

YESU ANAVYOLITAZAMA KANISA LAKE-sehemu ya kwanza

Kabla Yesu hajawaambia wanafunzi wake mtazamo wake juu ya kanisa alijaribu kuwauliza wao wanamtazamaje.  “Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa nani?” (Mathayo 16:13). 
 Na Yesu akapewa majibu. Majibu tofauti-tofauti kutoka mitazamo yao tofauti-tofauti. Kulikuwa na hao waliosema Yesu ni Yohana Mbatizaji; wengine walisema Yesu ni Eliya; Yesu ni Yeremia; Yesu ni mmojawapo wa manabii. Bila shaka Yesu alihuzunishwa na majibu yao. Kwa sababu Yesu alikuwa zaidi ya Yohana Mbatizaji, Eliya, Yeremia, au nabii. 
Baadaye, Petro akamtuliza Yesu kwa jibu sahii: “Wewe ndiwe Kristo (Masihi-Mkombozi aliyetumwa na Mungu), Mwana wa Mungu aliye hai?” Haleluya! Hapo, hapo Yesu akampongeza akimwambia, una bahati, huo sio mtazamo wa kibinadamu, “mwili na damu havikufunulia hili, bali baba yangu aliye mbinguni”(fungu la 18). Kwa lugha nyingine, Petro kwa kuwa unanitazama kwa macho ya imani kama mwana wa Mungu na mkombozi, subiri nitakueleza watu wenye imani kama yako ninavyowatazama. Kaa chini basi nilitambulishe kanisa langu kwako kama ninavyolitazama. Yesu anapompongeza Petro kwa kumtambua; hamwiti Petro, isipokuwa anamwita Simoni Baryona, hilo ndilo jina lake alilopewa na wazazi wake. Petro ni jina la kupewa-“jina la ubatizo” (Yoh 1:42). Petro  lina maana katika kiyunani kama mwamba. Na katika kiaramaki (lugha mama ya Yesu na Petro) mwamba huitwa kefa. Kwa kuwa Yesu alikuwa anaongea na Petro kwa kiaramaki bila shaka Yesu aliongea hivi: “Wewe ndiwe Kefa (mwamba) na juu ya kefa (mwamba)  nitalijenga kanisa langu”
Ni kweli Simoni mwana wa Yona ni sawa na wanadamu wengine. Lakini hapa Simon ameonesha ukefa, upetro, umwamba. Na ninyi ni mashahidi, wengi wamechagua kuyumbishwa na upepo wa maoni ya watu kunihusu mimi. Wengi wameniona kama Yohana Mbatizaji, Eliya, Yeremia, na kama nabii tuu. Lakini hapa Simon amejibu kama Petro (jiwe); amekataa kusogezwa na maoni ya wengi, kama mwamba usivyosukumwa na upepo. Petro ni muumini wa kwanza kunikiri mimi kama Mwana wa Mungu. Imani ya Petro kwangu kama Masihi na Mwana wa Mungu ni mwamba imara na salama ambao juu yake nitalijenga kanisa langu. 
 Na hapo labda unataka kujua, Je! Yesu alijenga kanisa lake juu ya imani ya Petro? Ni kweli kanisa leo linasimama juu ya imani ya mtume Petro:
·Katika mathayo 16:16 Petro ni wa kwanza kumkiri Yesu kama Mwana wa Mungu.
·Katika Matendo sura ya 2 Petro ndio wa kwanza kumtangaza Yesu kama Masihi na Mwana wa Mungu kwa Wayahudi
·Na katika Matendo sura ya 10 tunamkuta Petro tena kama mhubri wa kwanza wa Yesu kama Masihi na Mwana wa Mungu kwa Wamataifa.

Kwa kifupi wayahudi kwa wamataifa wanaikiri imaini ile ile ya Petro kwa Yesu. Kama Petro wakristo leo: 
·Tunaamini Yesu ni Masihi na Mwana wa Mungu hata kama wengine hawaamini hivyo.
·Leo hii tunaamini Yesu ni Masihi aliyetumwa na Mungu kutukomboa hata kama wengine hawamuoni hivyo. 
·Tunamwona Yesu kama Mungu mwenye nguvu hata kama wengine wanamwona ni mwana wa Mariam tu. 

Na ni imani hii ndio inayotufanya tusalie salama kama jengo lililosimama mwambani. Imani hii na mtazamo huu ndio mwamba. Msingi wa maoni ya wengi kuhusu Yesu kama nabii tu, mwalimu tu hautufai kusimamisha imani yetu juu yake. Misingi hiyo haitulii kama mchanga wa mwambao. Leo ipo kesho imechukuliwa na maji. Tunaposongwa na mitazamo tofauti tofauti juu ya Yesu ni muhimu kutoyumbishwa kama Petro. Na tukisimamia katika imani ya Petro tuko salama.

Hivyo, mbele ya macho ya Yesu kanisa la Mungu ni Jengo linalosimama juu ya mwamba wa imani. Ndivyo linavyosimama mbele ya macho ya Yesu.

ENDELEA KUJIFUNZA MTAZAMO WA YESU KWA KUNDILAKE  DUNIANI. ROHO WA BWANA AWE PAMOJA NAWE.AMINA

Monday, June 9, 2014

KUWEKWA HURU NA ILE KWELI-sehemu ya pili

 KUTAMBUA KUNDI LA MUNGU DUNIANI
Mamlaka za kiserikali hutuambia ya kwamba ni rahisi sana kutofautisha kati ya noti ya fedha ya
kweli na ile ya bandia. Unaona, wao hujifunza tabia ya ile note ya kweli kwa undani.Wanajua wembamba na mpangilio wa vijinyuzi vidogo sana vitengenzavyo karatasi, wepesi au uzito wa rangi au wino, nembo na utaratibu halali wa nambari za fedha iliyo halisi na ya kweli. (elezea fedha)! Wanapoitizama noti,
wanalinganisha upesi na zile sifa zitambulishazo fedha iliyo halali. Kama inapungukiwa sifa yoyote katika zile zilizo katika iliyo halali, basi inakuwa bandia.
Vivyo hivyo na kweli.
Hatuhitaji kujifunza mafundisho ya madhehebu yote kwa muda mrefu, kama tunajua tabia za kanisa la kweli la Mungu kama zilivyotajwa katika Biblia.!
Mungu hamuachi mwanadamu akisie kuwa ni ipi dini ya kufuata, kwani Mungu ametupatia kweli katika Neno lake: Hakika Bwana MUNGU !hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.!Amosi 3:7
Kitabu cha Ufunuo ni muhtasari wa unabii wote katika Biblia. Kinawapatia watu mtizamo wa pekee wa siku ya mwisho.!Hapa mchafuko wa uasi na dini uliopo katika siku za mwisho za historia ya Dunia unafunuliwa.!
Ufunuo unatabiri juu ya pambano kati ya kanisa la Kristo na Shetani.!Sura ya 12 inatoa picha kama filamu ya historia ya kanisa tangu wakati wa Kristo hadi mwisho wa dunia:

NEEMA YA BWANA WETU YESU KRISTO IWE PAMOJA NAWE, NA BWANA ATUFUNULIE KWELI YOTE KWA MSAADA WA ROHO MTAKATIFU.AMINA.

Sunday, June 8, 2014

KUWEKWA HURU NA ILE KWELI-sehemu ya kwanza

Tangu mwanadamu alipochagua kufuata njia yake katika Bustani ya Edeni, amekuwa na  utupu usio wa kawaida ambao Mungu mwenyewe aweza kuujaza.Mungu aliwaruhusu wana wa Israeli katika kutanga kwao jangwani wawe na njaa ili wapate kutambua hitaji lao la kuwa naye.!Mungu alinena na Wana wa Israeli kupitia kwa Musa,akisema (Fungu: KumbukumbulaTorati8:3)!Akakutweza, akakuacha uone njaa,.....apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu;bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha BWANA.!Ni wazi Mungu huturuhusu tuhisi njaa ya ndani nakuchoka, ili tumfikie na tumruhusu Mungu aridhishe tamaa zetu. Leo, tunaona tamaa kubwa katika namna mbalimbali za dini.!Pamoja na msisitizo mkubwa leo katika swala la  muungano wa dini na msukumo wa kuvunja kuta za kimadhehebu, kuna majifunzo mengi zaidi na mawazo yahusuyo aina mbalimbali za dini na za kanisa. Makanisa mapya yanaibuka kwa kasi zaidi katika dunia.!Kila moja linadai kuwa watu wa pekee wa Mungu likiwa na ujumbe wa kweli kwa ajili ya kila mtu duniani.!Bado hayo madai yanapotafakariwa itahakikishwa wazi ya kwamba si madai yote yawezayo kuwa ya kweli.Kila moja linadai kuwa Biblia ndiyo msingi wa imani yao, lakini mafundisho yao ni ya tofauti sana.Yawezekanaje watu waaminifu kuchambua madai yote haya ya dini hizi na kujua kwa hakika kwamba kweli ni nini.!Je, Mungu kweli analo kundi la pekee katika Ukristo analolitambua kama kanisa lake leo?!Ni wazi hivyo, kwani Paulo aliandika:(Fungu: Waefeso 4:4)!Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote.....!Waefeso 4:4-6
(Fungu: 1 Timotheo 3:15)!Paulo aliandika kwa rafiki yake kijana, Timotheo, na kusema, ....upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu,iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli.!1 Timotheo 3:15.!Paulo anataja wazi ya kwamba kanisa la Mungu leo ni nguzo na msingi wa kweli, lakini je, tunawezaje kugundua kanisa lipi linao ukweli.Yapo madhehebu mengi sana, mapambano mengi sana, kuchanganyikiwa kwingi sana katika jumuiya ya kidini.Marafiki, kulingana na maandiko, Yesu kamwe hakukusudia ya kwamba kuwepo kuchanganyikiwa kwokwote, na ni wazi pia hakukusudia kuwepo madhehebu yote haya.!Kabla tu ya kusulubishwa, Yesu alisali:(Fungu: Yohana 17:21)!Wote wawe na umoja, kama wewe, Baba, ulivyo   ndani yangu, nami ndani yako;hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.!Yohana 17:21.!Yesu alitaka ulimwengu uweze kutambua wafuasi wake kwa njia ya umoja wao na upendo.!Kristo hakutaka migawanyiko ya namna yoyote ndani ya kanisa lake.Kwa kweli, Paulo aliandika ya kwamba kusiwe na faraka (mgawanyiko) katika mwili.!1 Wakorintho 12:25.
Lakini Paulo alisema ya kwamba uasi ungekuja, na pamoja na huo, mgawanyiko!(Fungu: Matendo 20:28 - 30)!Tunasoma: Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo.........mpate kulilisha kanisa lake Mungu....Najua mimi ya kuwa !baada ya kuondoka kwangu mbwa mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi.Tena katika ninyi wenyewe !watainuka watu wakisema mapotovu,wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.!Matendo 20:28-30. 

Tunapofungua kurasa za historia ya kanisa,tunagundua hili ndilo hakika lililotokea.!
Waalimu wa uongo waliinuka, na baadhi wakapokea makosa yao na kuliacha kanisa.!Wengine wakachanganyikiwa. Wanafunzi wakavutwa mbali, na kukawa na kuanguka pole pole toka katika
mafundisho ya Yesu.!Lakini hata kupitia katika yote hayo, bado Mungu amekuwa na kanisa lililosalia kuwa aminifu.Lakini baadhi ya watu husema, Yaweza kuchukua muda wa maisha yote kujifunza mafundisho ya kila dini ili kupata kuwa ni lipi ni kanisa la kweli laMungu.!Lakini ipo njia rahisi.!Njia ya Mungu!


ENDELEA KUTEMBELEA BLOG HII UPATE KUJIFUNZA NJIA YA MUNGU YA KULITAMBUA KANISA LA KWELI LA MUNGU.

Wednesday, June 4, 2014

KUJIPATIA MARAFIKI WA AINA MBALIMBALI

Marafiki ni sehemu muhimu sana ya maisha ya mtu yeyote. Watu wengi wameanguka ama kuinukia kutokana na marafiki.
Chumvi inayowawezesha watu kuishi vizuri katika kundi la aina yoyote ni kupendana na kusaidiana, yaani kuwa marafiki kwani Rafiki ni mtu mnayefahamiana,mnayezoeana na kupendana.

MBINU ZA KUANZISHA AU KUTAFUTA MARAFIKI:
-Ukitaka fulani awe rafiki yako basi chukua muda wa kujifunza habari zake kama vile mambo anayopendelea n.k kisha tafuta nafasi ya kukutana na kuongea naye kila mara fursa ya kufanya hivyo inapojitokeza.
-Ikiwa unataka uzungukwe na marafiki wa kweli wakati wote ni lazima ujitahidi kurekebisha tabia yako ili ivute wenzako na kuwafanya wakuthamini na kukuamini.
-Ili watu wavutwe kwako, inatakiwa uonyeshe tabia ya uchangamfu kiasi, usawa, ukweli na nia ya kunufaisha wengine.

MARAFIKI WANA FAIDA GANI?
kuna faida nyingi mbalimbali ambazo mtu ataweza kuzipata kutokana na aina za marafiki alio nao. Kwa mfano rafiki aliye mwandani wake atamfaa sana kwa kuchangamkiana,kuendelezana n.k. Rafiki aliye ahi au sahib wake anakuwa kama ni nguzo yake inayomtegemeza na kumwunga mkono katika mambo yake mengi mbalimbali.Rafiki aliye shoga au mwenzi wake ataweza kumwondolea upweke na wakati huo huo kumpatia nafasi nzuri ya mazoezi kuhusu jinsi ya kuishi na wengine katika uhusiano wa karibu sana.Rafiki aliye somo wake ataweza kumpa ushauri kuhusu mambo mbalimbali yenye manufaa; na rafiki muhimu,ambaye kwa kawaida huwa ni mchumba au mme/mke huongeza furaha na kusaidia katika kutayarisha mambo mbalimbali yaliyo msingi wa maisha ya baadaye.Marafiki wengine wote wa kawaida wenye tabia njema na upeo wa mambo mbalimbali ya kimaisha katika nyanja za kiroho,kiakili na kimwili watasaidia maendeleo na ustawi wetu katika nyanja hizo walizobobea.
RAFIKI WA KWELI NI YUPI?
Rafiki wa kweli ni yule mwenye upendo wa kweli unaojidhihirisha katika kukutakia mema na katika kujali maslahi yako. Kwa kawaida rafiki kama huyo hakuongopei wala hana sura ya kinyonga-yaani hajipendekezi kwako wakati mkiwa pamoja na kukusengenya unapotupa kisogo. Yu mwaminifu kwako katika kila hali. Sio rahisi kupambanua marafiki wa kweli na wala sio rahisi kuwapata wengi wa aina hii.

Ni matumaini yangu kwamba baada ya kusoma maelezo haya mafupi kuhusu marafiki, utaanza kupata nuru mpya ya kuwatazama rafiki zako .
Kwa kukariri ningependa usiache kuzingatia yafuatayo:-
  • Jipatie marafiki -wavulana/wanaume kwa wasichana/wanawake.
  • Wachague vizuri marafiki hao kutokana na tabia zao njema na manufaa yao kwako.
  • Wewe mwenyewe jitahidi uwe mwenye tabia njema, mwenye manufaa kwa rafiki zako, na mwaminifu kwa kila mmoja wao, kadri ya uwezo wako wote.
  • Jitahidi kuwafanya watu wenye tabia zisizokubalika katika jamii kuwa marafiki zako kwa kuwabadilisha tabia zao kwa hekima na upole kama Yesu alivyofanya wakati wa maisha yake hapa duniani.Yesu aliwabadilisha watoza ushuru wezi kama Zakayo,makahaba kama Mwamamke msamaria n.k kuwa marafiki wake.
UBARIKIWE NA BWANA UNAPOENDELEA KUJIFUNZA KWA YESU NAMNA MBALIMBALI ZA KUJIPATIA MARAFIKI KAMA YEYE MWENYEWE ALIVYOFANYA KAMA KIELELEZO CHETU. 

KUSOMA NENO LA MUNGU KWA UONGOZI WA ROHO MTAKATIFU

NAWASALIM NYOTE KTK JINA LA BWANA WETU YESU KRISTO. KATIKA KUMJUA MUNGU TUNA MAMBO MENGI AMBAYO YATUPASA TUYAJUE BILA KUDANGANYIKA AU KUDANGANYWA. HAYA YOTE TUNAYAPATA KWA KUSOMA BIBLIA TAKATIFU KUANZIA KITABU CHA MWANZO HADI UFUNUO KWA UONGOZI WA ROHO MTAKATIFU ALIYEWAVUVIA MANABII NA MITUME WA MUNGU KUANDIKA VITABU VYA BIBLIA.

MASWALI HAYA NILIPATA MAJIBU SAHIHI BAADA YA KUSOMA BIBLIA KWANI NILIVYOKUWA NAJUA NI TOFAUTI NA BIBLIA INAVYOSEMA. NAWE NDUGU YANGU SOMA NAWE UPATE KUJUA UKWELI ILI USIJE WAOMBA WAFU KAMA WAPAGANI WAFANYAVYO.
JE, WAFU WAKO WAPI?
WENGI TUNAJUA WAPO MBINGUNI AU MOTONI? LA HASHA! WAFU WAPO KUZIMU AU TUNAWEZA KUSEMA WAPO MAKABURINI. SOMA MHUBIRI 9:5-6,10, AYUBU 19:25-27,YOHANA  5 :28-29.


JE, SIKU YA MWISHO NI AKINA NANI WATAFUFULIWA?
WALE WALIOKUFA KATIKA KRISTO WATAFUFULIWA KWA UFUFUO WA UZIMA NA WALE WALIOTENDA MABAYA KWA UFUFUO WA HUKUMU SOMA YOHANA 5:28-29, MATENDO 24:15.


UBARIKIWE KWA KUENDELEA KUJIFUNZA UKWELI KUHUSU MASOMO MBALIMBALI YA BIBLIA.

Saturday, May 31, 2014

KUJIJENGEA TABIA YA KRISTO

"MJIFUNZE KWANGU" 
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu.
Mathayo 11:29.
"Mjifunze kwangu," alisema yule Mwalimu wa Mbinguni, "kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo...." Yatupasa kujifunza kujikana nafsi, yatupasa kujifunza ujasiri, saburi, ushupavu, na upendo unaosamehe.... Iwapo tunayo imani ndani ya Yesu kama msaidizi wetu, iwapo macho yetu ya imani
yanaelekezwa kwake kila wakati, basi,tutakuwa kama Yesu katika tabia zetu. Atakaa ndani ya mioyo yetu, nasi tutakaa ndani yake Kristo. Tukiwa tumevikwa haki ya Kristo, maisha yetu yanafichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Atakuwa mshauri wetu. Tukimwomba kwa imani, atatufungua ufahamu wetu.... Mafundisho aliyotupa Kristo yatawekwa katika matendo. 
Kristo, Kielelezo Chetu, anapowekwa daima mbele ya macho ya akili zetu, hapo ndipo tabia mpya zitaweza kukuzwa, mielekeo yetu mibaya yenye nguvu tuliyorithi pamoja na ile tuliyojizoeza wenyewe itaweza kudhibitiwa na kushindwa, kujisifu kwetu kutatupwa mavumbini, tabia mbaya za zamani za mawazo zitapingwa daima, kupenda kwetu makuu
kutajionyesha katika tabia yetu kwa dhahiri na kudharauliwa, nasi tutakushinda. 
Kristo hana budi kuingia katika mawazo yetu yote, hisia zetu zote, na mapenzi yetu yote.
Anapaswa kutukuzwa katika mambo madogo sana ya utumishi wetu wa kila siku katika kazi ile aliyotupa kufanya. Wakati tunapoketi miguuni pake Yesu, badala ya kutegemea
ufahamu wetu wa kibinadamu au kufuata maneno ya hekima ya ulimwengu huu,tunapaswa kuyapokea maneno yake kwa shauku, tukijifunza kwake, na kusema, "Bwana,wataka mimi nifanye nini?" hapo ndipo hali yetu ya asili ya kujitegemea wenyewe, yaani,
kujitumainia wenyewe, kufuata mapenzi yetu wenyewe, itabadilika, na mahali pake itakuwapo roho ile ya kitoto, tiifu, inayokubali kufundishwa. Tunapokuwa na uhusiano sahihi na Mungu wetu, tutaitambua mamlaka ya Yesu katika kutuongoza sisi, na madai
yake kwetu kwamba tumpe utii usiokuwa na maswali.
Tutakuwa na mawazo ya hali ya juu kumhusu Yesu Kristo hata nafsi zetu zitajishusha chini. Mapenzi yetu yatakuwa ndani ya Yesu, mawazo yetu yatavutwa kwa nguvu kuelekea mbinguni. Kristo atakuwa hana budi kuzidi, wakati MIMI NINAPUNGUA....
Tutajizoeza kuwa na wema ule ulio ndani yake Kristo, ili sisi tupate kuakisi kwa wengine mfano wa tabia yake. 

KUJITIA NIRA YA KRISTO 
Kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi. Mathayo 11:30.
Kujitia nira ya Kristo, maana yake kufanya kazi kulingana na njia zake, kuwa mshirika mwenzi pamoja naye katika mateso yake na taabu zake kwa ajili ya wanadamu waliopotea.
Katika kuikubali nira yake Kristo ile ya kujizuia na utii, utaiona kwamba imekuwa msaada mkubwa sana kwako. Kujitia nira hii kunakuweka wewe karibu na ubavu wake
Kristo, naye anachukua sehemu ile iliyo nzito kuliko zote ya mzigo huo. 
Nira na msalaba ni nembo zinazowakilisha jambo lile lile moja ----- kusalimisha mapenzi [nia] yetu yote kwa Mungu. Kujitia nira kunamwunganisha mwanadamu katika urafiki pamoja na yule mpendwa sana Mwana wa Mungu. Kuuinua msalaba juu
kunaiondoa nafsi moyoni, na kumweka mwanadamu mahali ambapo anajifunza kubeba mizigo yake Kristo. Hatuwezi kumfuata Kristo bila kujitia nira yake, yaani, bila kuuinua juu msalaba wetu, na kujitwika na kumfuata. Kama mapenzi yetu hayapatani na matakwa yale ya mbinguni, basi, inatupasa sisi kuyakataa matakwa yetu, kuachana na tamaa zetu tunazozipenda sana, na kukanyaga katika nyayo zake Kristo....
Wanadamu hujitengenezea nira ambazo huonekana kuwa ni nyepesi na za kupendeza kuvaa kwa ajili ya shingo zao wenyewe, lakini matokeo yake ni kwamba zinachubua vibaya mno. Kristo analiona jambo hilo, na kusema, "Jitie nira yangu. Nira ile unayoweza kuitia shingoni mwako, ukidhani inakufaa sana, haitakufaa hata kidogo. Jitie nira yangu, nawe ujifunze kwangu mafundisho ambayo ni ya muhimu kwako kujifunza." 
Kazi yako sio kukusanya mizigo yako mwenyewe.... Mara nyingi sisi tunafikiri kwamba tuna wakati mgumu katika kuibeba mizigo yetu, na mara nyingi mno mambo yanakuwa hivyo, kwa sababu Mungu hajaweka mpango wo wote kwa ajili yetu kuibeba mizigo
hiyo; lakini tunapojitia nira yake na kuibeba mizigo yake, hapo ndipo tunaweza kushuhudia kwamba nira ya Kristo ni laini na mizigo yake ni myepesi, kwa sababu yeye ameweka mpango wa kuibeba hiyo [mizigo yake].
Hata hivyo, nira hiyo haitatupatia sisi maisha ya raha na uhuru na kujifurahisha nafsi zetu. Maisha yake Kristo yalikuwa ni maisha ya kujitoa mhanga na kujikana nafsi kwa kila hatua [aliyokwenda]; na kwa upendo unaodumu daima kama ule wa Kristo, mfuasi
wake wa kweli atatembea katika nyayo za Bwana wake; naye atakapokuwa anasonga mbele katika maisha haya, atazidi kujazwa na roho ile ile na maisha yale yale ya Kristo. 

TUKIJIKANA NAFSI,NAFSI ZETU ZITAKUFA NA NAFSI YA KRISTO ITAISHI NDANI YETU.


UJUE MOYO WAKO-sehemu ya tatu

NGUVU HALISI YA NIA 
Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo. 2 Wakorintho 8:12.
Dini iliyo safi inahusika na matumizi ya nia. Nia ni uwezo unaotawala katika maumbile
ya mwanadamu, ikiuleta uwezo mwingine wote uliomo mwilini chini ya mamlaka yake.
Nia si kuonja wala mwelekeo, bali ni uwezo wa kuamua la kufanya ambao unafanya kazi
yake ndani ya wana wa wanadamu ama ukiwaelekeza kwenye utii kwa Mungu, ama kwenye uasi....
Bila shaka wewe unatamani kuyafanya maisha yako kuwa kama vile ambavyo yangefaa kukuwezesha kuingia mbinguni hatimaye. Mara nyingi unakata tamaa unapojiona mwenyewe kuwa u dhaifu katika uwezo wako wa kimaadili [tabia], unajikuta u mtumwa wa mashaka, tena umetawaliwa na tabia na desturi za maisha yako ya zamani ya dhambi.... Ahadi zako [maazimio yako] ni kama kamba zilizotengenezwa kwa mchanga....
Daima utakuwa hatarini mpaka hapo utakapoielewa nguvu halisi ya nia yako. Unaweza kuamini na kuahidi mambo yote, lakini ahadi zako au imani yako haina maana yo yote
mpaka hapo utakapoiweka nia yako nyuma ya imani yako na nyuma ya matendo yako.
Kama wewe unapiga vita ile ya imani kwa uwezo wako wote wa nia yako, utashinda.
Hisia zako, mvuto wako, mapenzi yako ya moyoni, mambo yote hayo hayaaminiki, kwa sababu hayawezi kutegemewa....
Lakini wewe huna haja ya kukata tamaa.... Ni juu yako mwenyewe kuisalimisha nia yako kwa nia ile ya Yesu Kristo; nawe unapofanya hivyo, Mungu atakushika mara moja na kufanya kazi yake ndani yako ili upate kutaka na kutenda yale yampendezayo Yeye.
Mwili wako wote ndipo utakuwa chini ya utawala wa Roho wake Kristo, na hata mawazo yako yatatawaliwa naye. Huwezi kuzitawala hisia zako, wala mapenzi yako ya moyoni, kama unavyotaka mwenyewe; lakini unaweza kuitawala nia yako [maamuzi yako], nawe kwa njia hiyo unaweza kufanya mabadiliko kamili katika maisha yako. Kwa kuisalimisha nia [mapenzi] yako kwa Yesu, maisha yako yatafichwa pamoja na Kristo katika Mungu na kuunganishwa na mamlaka ile ipitayo falme zote na mamlaka zote.
Utakuwa katika nguvu yake; na nuru mpya, yaani, nuru ile ya imani iliyo hai, itawezekana kwako kuwa nayo. Lakini nia yako ni lazima ishirikiane na nia yake Mungu....
Je! wewe hutasema, "Nitampa Yesu nia yangu, nami nitafanya hivyo sasa hivi," na kuanzia dakika hii hutakuwa upande wake Bwana kabisa? 

Thursday, May 29, 2014

UJUE MOYO WAKO-sehemu ya pili

KUJIANDAA KWA SHULE ILE YA JUU ZAIDI

Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana wewe ndiwe Mungu wa wokovu
wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa. Zaburi 25:5.
Wale ambao ni wana wa Mungu hapa duniani wanaketi pamoja na Yesu katika Shule ya
Maandalizi, wakijitayarisha kupokewa katika Shule ile ya Juu Zaidi. Siku kwa siku
tunatakiwa kila mmoja kufanya maandalizi yake mwenyewe; maana katika majumba yale
ya kifalme kule juu hakuna ye yote atakayewakilishwa na mtu mwingine. Kila mmoja
wetu anapaswa kuusikia yeye mwenyewe mwito ule usemao, "Njoni kwangu,... nami
nitawapumzisha...."
Bwana Yesu amekulipia ada ya mafundisho. Yote yakupasayo kufanya ni kujifunza
kwake.
 Upole kama ule wa Kristo utakaoonyeshwa kwa matendo katika Shule ile ya Juu
unatakiwa kuwekwa katika matendo na wakristo wote, wazee kwa vijana, katika Shule
hii ya Chini. Wale wote wanaojifunza katika shule hii ya Kristo wako chini ya mafunzo
wakiongozwa na wajumbe wale wa mbinguni [malaika]; wala haiwapasi kamwe kusahau
ya kwamba wao ni tamasha kwa ulimwengu huu, kwa malaika, na kwa wanadamu.
Wanapaswa kumwakilisha Kristo. Wanatakiwa kusaidiana wenyewe ili waweze kufaa
kuingia katika Shule ile ya Juu zaidi. Wanapaswa kusaidiana kila mmoja na mwenzake ili
wapate kuwa watakatifu na wenye utukufu, na kulizingatia sana wazo lile la kweli
linaloonyesha maana ya kuwa mtoto wa Mungu. Wanapaswa kusema maneno ya kutia
moyo. Wanapaswa kuiinua juu mikono iliyo dhaifu na kuyafanya imara magoti
yaliyolegea. Juu ya kila moyo panatakiwa kuandikwa maneno haya, kana kwamba ni kwa
kalamu yenye ncha ya almasi, "Hakuna kitu cho chote ninachokiogopa, isipokuwa tu
kwamba mimi sitaujua wajibu wangu, au nitashindwa kuutekeleza."...
Moyo uliodhibitiwa, maneno ya upendo na upole, humletea heshima Mwokozi wetu.
Wale wasemao maneno ya upole, maneno ya upendo, maneno yaletayo amani,
watatunukiwa vizuri sana.... Tunapaswa kumruhusu Roho wake kuangaza katika maisha
yetu ya nje ule upole na unyenyekevu wa moyo tuliojifunza kwake.
Yesu ndiye Mwalimu wetu Mkuu.... Anapenda sana, tena yu tayari sana kukuchukua
wewe katika ushirika wa karibu sana na Yeye mwenyewe. Yu tayari kukufundisha jinsi
ya kuomba kwa imani yenye matumaini na uhakika kama ile ya mtoto mdogo.
Jiandikishe upya jina lako kama mwanafunzi wa shule yake. Jifunze kuomba kwa imani.
Pokea maarifa yake Yesu.
Je! wewe huwezi kuketi miguuni pake Yesu na kujifunza kwake?

MUNGU ATUVUTE KWAKE TUJIFUNZE KWAKE KWANI YEYE NI MNYENYEKEVU WA MOYO.


UJUE MOYO WAKO...sehemu ya kwanza

KUJIFUNZA KATIKA SHULE YA KRISTO 
Ni nani amchaye BWANA? Atamfundisha katika njia anayoichagua. Zaburi 25:12.

Yesu amefungua shule kwa ajili ya kuwaelimisha na kuwapa mazoezi wateule wake, nao wanapaswa kuendelea kujifunza daima kuyaweka katika matendo mafundisho yale anayowapa, ili wapate kumjua kabisa.
Wale wanaofikiri kwamba wao ni wema kiasi cha kutosha, wala hawafanyi kazi kwa bidii katika kuikamilisha tabia yao ya Kikristo, wataweka sanamu mioyoni mwao, nao wataendelea kutenda dhambi katika maisha yao mpaka dhambi kwao itaonekana kuwa si
dhambi tena....

Yesu anajitoa nafsi yake kwa kila mtu aliye mgonjwa, kwa kila mtu anayejitahidi kushinda. Roho Mtakatifu anamwombea kila mpiga mweleka mwaminifu, naye Kristo atayafanya maneno yake kuwa roho na uzima, yaani, kuwa uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila mtu aaminiye. Lakini wewe utashindwa kabisa utakapomruhusu yule mwovu kuutawala moyo wako, yaani, kuyaongoza mawazo yako.... Mungu hatadhihakiwa; hataukubali moyo uliogawanyika. Yeye anataka tumpe huduma yetu yote
kwa moyo wetu wote. Amelipa fedha ya fidia yetu kwa kujitoa nafsi yake mwenyewe kwa ajili ya kila mwana na binti ya Adamu....
Kristo anayo madai juu ya kila mtu; lakini wengi huchagua maisha ya dhambi. Wengine hawataki kuja kwa Yesu ili awape uzima. Wengine husema, "Naenda, Bwana," kwa
mwaliko wake, lakini hawaendi; hawajisalimishi nafsi zao kabisa ili kukaa ndani ya Yesu peke yake, ambamo ni uzima na amani na furaha isiyoneneka, yenye utukufu.... Je! hatutaamka na kuwa na hekima na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya umilele? tafuteni
neema yake Kristo kwa moyo  wote, kwa uwezo  wote, na kwa nguvu  zote.

Mungu ametupa  haki ya kumshikilia Yeye kwa njia ya maombi ya imani. Maombi yaliyojaa imani ndicho kiini cha dini safi, ni nguvu ya siri aliyo nayo kila Mkristo.
Tafuta muda wa kuomba, kuyachunguza Maandiko, kuiweka nafsi yako chini ya nidhamu ya Yesu Kristo. Uishi kwa kuwasiliana na Kristo aliye hai, na mara tu unapofanya hivyo, atakuchukua na kukushika kwa mkono wake ulio imara ambao hautakuachilia kamwe.

UBARIKIWE UNAPOFANYA MATENGENEZO KWA KUUJUA MOYO WAKO NA NEEMA YA BWANA WETU YESU KRISTO IWE NAWE DAIMA.

Wednesday, May 28, 2014

UNAWEZAJE KUMKANA KRISTO?

  • Tunaweza kumkana kwa maneno yetu na kwa kusema mabaya juu ya wengine kwa mazungumzo ya upuzi, ubishi na maneno ya mzaha.
  • Kwa maneno ya bure, yasiyo na maana au maneno makali ama kwa kusema uongo, kinyume cha kweli. kwa maneno yetu tunaweza kuonyesha kuwa kristo hayupo ndani yetu.
  • Kwa tabia yetu tunaweza kumkana Kristo kwa kupenda raha ,kwa kuepuka kazi na mizigo ya maisha ambayo mtu mwingine hana budi kuichukua kama sisi tusipoichukua.
  •  Kwa kiburi cha nguo tuvaazo ,kwa kufuata mtindo wa ulimwengu au kwa mwenendo mbaya usio na adabu. 1Petro3:3-5.
  • Kwa kupendelea maoni yetu wenyewe na kujaribu kuudumisha utu wa kale au kujihesabu wenyewe kuwa wenye haki.

Usalama tu kwa vijana ni kukesha kila wakati na kuomba kwa moyo mnyenyekevu. Kama twafanya hivyo malaika hutazama sala zetu, na ikiwa sala hizo hazijatoka katika midomo ya kusingizia wakati tukiwa katika hatari ya kufanya mabaya bila kujua na kutoa mvuto utakaowaongoza wengine kufanya mabaya, malaika atulindae atakuwa karibu nawe  kukusaidia kutenda mema, akikuchagulia maneno, na kuongoza matendo yako.Zaburi 5:3-4 .
soma Mithal 3:3-4, 2Timotheo 2:19, Waebrania 12:14.

Tuesday, May 27, 2014

MBINU NA KANUNI ZA KUISHI NA WATU VIZURI

-Uwe na tabia ya kupenda watu kwa moyo wote. Mathayo 22:39
-Heshimu kila mtu na kila mtu umwone ni mtu muhimu. 1petro 2:17
-Usidharau mtu yeyote. mithali 13:1
-Usiwe msengenyaji na usiseme watu vibaya. 7:1-5
-Usipende kugombeza au kutukana watu. Tito 3:2
-Shukuru kwa kila jambo jema linapotendeka. 1Thesalonike 5:18
-Usiwe mtu mwenye kujipendekeza kwa watu. Mithali 29:5
-Uwe mnyenyekevu na usijivune kwa lolote lile, acha wengine wakusifu. 1petro 5:5
-Usiwe na kinyongo , fitina na usitunze chuki. mambo ya walawi 19:17-18
-Jipende na kujikubali kama ulivyo kimaumbile na uwezo wako, ndipo na watu watakupenda na kukubali kama ulivyo. mithali 19:8
-Usimharibie au kumchafulia mtu jina lake. walawi 19:16
-Usiwe na wivu juu ya mafankio ya wengine. yakobo 3:16
-Ukitaka watu wakuheshimu jiheshimu wewe kwanza. mathayo 7:12
-Usimcheke mtu mwenye shida, kasoro au anapokosea. 2wafalme 2:23
-Usiwe na tabia ya kukumbushakumbusha mtu makosa yaliyopita. mika7:19
-Kubali kikomo cha uwezo wa binadamu katika mambo fulani fulani na elewa kuwa hakuna aliye kamili kwa kila kitu. yakobo 3:2

KAMA UNATABIA FULANI MBAYA, MWOMBE MUNGU ATAKUSAIDIA NA KUJISAHIHISHA.

UZURI WA KITU UPO KATIKA MACHO YA MWONAJI

Watu wana mitazamo mbalimbali.
 Hata kuhusu kanisa watu wanaliangalia  tofauti tofauti.
 Kanisa linaweza kuonekana vizuri kwa macho ya mmoja ila kwa mwingine likaonekana vibaya. Tofauti ipo machoni, kwani uzuri wa kitu upo katika macho ya mwonaji:
Kwa mwingine kanisa ni mgodi wa hazina ya milele huku wengine  kanisa ni shimo lililojaa mapokeo ya zamani (uzuri wa kitu upo katika macho ya mwonaji)                
  Kwa mwingine kanisa la Lutherani ndio kanisa na huku kwa mwingine Katoliki ndio kanisa (uzuri wa kitu upo katika macho ya mwonaji).
   Tena kwa mwingine kanisa ni Wapentekoste na kwa mwingine ni Wa Sabato (uzuri wa kitu upo katika macho ya mwonaji).
Lakini macho yetu sio kiongozi amini. Leo yananionesha mwanamke yule kuwa anapendeza. Kesho yananionesha mwingine na kunifanya nipoteze hamu na wa jana. Hata kanisa nililoliona jana limejaa ngano leo naliona limejaa magugu tupu. Macho yetu si kiongozi wa kuaminika, hayatulii.

Macho ya Kristo pekee hayachezi-chezi. Yanatulia yanapotazama. Zaidi ya tochi macho ya Yesu yanapenya ngozi nakufika mpaka moyoni. Yanaona uzuri na udhaifu uliofichika. Mtazamo wa Mungu ni sahii. 

TEMBELEA BLOG HII UPATE KUJIFUNZA MTAZAMO WA KRISTO JINSI ULIVYOFUNULIWA KATIKA BIBLIA ILI KWA NEEMA YA MUNGU UWEZE KUWA NA MTAZAMO KAMA WA YESU KRISTO.




Monday, May 26, 2014

MTU HUPIMWA KWA MAMBO MAKUU MATATU...!

NAMNA ANAVYO VAA: Mavazi ni moja ya kipimo cha nje kinachothihirisha falsafa na staha ya mvaaji. Kabla ujavaa vazi lako, jiulize kama vazi hilo ni la heshima, kikahaba n.k.

NAMNA ANAVYO ONGEA: Kwa kawaida mtu huongea yaliyo ujaza moyo wake, Hivyo tunavyozungumza kuna onyesha jinsi tulivyo.Kabla hujaongea jiulize Kama ingekuwa ni Yesu yuko katika mazingira yako angeweza kutamka maneno kama yako?

NAMNA ANAVYO KULA: Je ni mroho wa chakula au la! Inatupasa tujiulize kama tunadhamini chakula kuliko mambo ya kiroho au utu?


TUMTAZAME YESU KATIKA KILA JAMBO TUFANYALO NASI TUTAKUWA SALAMA KWANI YEYE PEKE YAKE NDIYE KIELELEZO CHETU KATIKA USAFI WA ROHO.

Sunday, May 25, 2014

KUWAITA VIJANA KUMCHA MUNGU

KUWAITA VIJANA WOTE!
Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana MUNGU, Tumaini langu tokea ujana wangu. Zaburi 71:5.
Yesu anamwita kila mpotevu, akisema, "Mwanangu, nipe moyo wako." Mithali 23:26....
Vijana hawawezi kuwa na furaha bila kuwa na upendo wa Yesu. Anangoja kwa huruma
kusikiliza maungamo ya wale walio watundu, na kuikubali toba yao. Anatazamia
kurudishiwa shukrani toka kwetu, kama vile mama anavyotazamia kuona tabasamu ya
kumtambua toka kwa mtoto wake ampendaye sana. Mungu aliye mkuu anatufundisha sisi
kumwita yeye Baba. Angependa sisi tuelewe jinsi moyo wake kwa dhati na kwa upole
unavyotupenda sana tunapokuwa katika maonjo na majaribu yetu....
Vijana wangekuwa wanaendelea daima kukua katika neema, na katika ujuzi wa ile
kweli. Muumbaji wa vitu vyote, ambaye hazina zote za hekima anazo, ameahidi kuwa
kiongozi wetu katika ujana wetu. Yeye aliyezishinda nguvu zote za uovu kwa ajili yetu
anatutaka tumsujudie. Hapawezi kuwapo na ujuzi wa juu kuliko ule wa kumjua Yeye
ambaye kumjua vema ni uzima na amani; hakuna upendo ulio safi na wenye kina kuliko
upendo ule wa Mwokozi wetu.
Kuna majaribu kila upande kuinasa miguu ya wale wasiojihadhari. Vijana wale
wasiomcha Mungu, wenye matendo mabaya wanao mvuto wenye nguvu kuwaongoza
wengine katika njia zile zilizokatazwa. Hao ni miongoni mwa vibaraka wa Shetani
wanaofanikiwa sana.... Mara nyingi wapenda dunia hii watakuja katika vazi la kirafiki, na
kujaribu kuingiza desturi na matendo yake. Hebu kila askari wa kweli awe tayari
kuvipinga vishawishi hivyo.
Shetani hutushambulia mahali pale tulipo na udhaifu; lakini hatuna haja ya kushindwa.
Shambulio hilo laweza kuwa kali na la muda mrefu, lakini Mungu ameahidi kutupatia
msaada wake, na kwa nguvu zake sisi tunaweza kushinda.... Kanuni na ahadi za neno la
Mungu zitatupatia silaha zenye uwezo wa Mungu kumpinga adui huyo.... Shetani
 atachanganyikiwa na kushindwa anapokuta moyo wako
unajishughulisha na kweli ya Mungu. Pia mara kwa mara tunahitaji kuonekana kwenye
kiti kile cha neema. Maombi ya bidii na ya kudumu, yakiunganisha udhaifu wetu wa
kibinadamu na Uweza usio na kikomo wa Mungu, yatatupatia ushindi.

SOMA HABARI ZINAZOCHAPISHWA KATIKA BLOG HII UPATE NURU KUTOKA MBINGUNI

Friday, May 23, 2014

UZITO WA NENO "NAKUPENDA" ~VIJANA WA KILEO

UJUMBE MAALUM KWA VIJANA.
UZITO WA NENO "NAKUPENDA"

Katika mawazo na fikra nyingi za vijana wa kileo neno, "NAKUPENDA" linatumika vibaya sana bila kuzingatia muda, mahali na hata kiwango au hadhi ya mtu unayemuambia kuwa unampenda.
Neno hilo limekuwa kama salamu tu, bila shaka ni kama mtu anaposema shikamoo! limekuwa ni kigezo kikubwa cha kuwalaghai wasichana kisha kuwachezea na baadaye kuwaacha. Wasichana wengi nao wanapotamkiwa neno "NAKUPENDA" wanachanganyikiwa kabisa, linawavuruga kabisa mfumo wa fahamu na kuwanyima uwezo wa kufikiri tena juu ya maisha yao ya baadaye kwani wanajiona wao ndio wao, kitakachofuata baada ya hapo ni "NAKUPENDA PIA" na baadaye neno "NDIYO" katika kila jambo.
Sasa basi, kwa nini wewe kijana wa kiume uliyelelewa na kufunzwa adabu njema, umtamkie msichana kuwa UNAMPENDA wakati huna uhakika na hisia zako na humaanishi unachokisema? Kwa nini basi usitumie neno "NAKUPENDA" wakati wa ndoa yako utakapowadia? Au kwa nini neno hili lisitumike katika kujenga mahusiano ya kawaida tu?
Tafakari kwa makini, unatakiwa kuwa na uhakika wa hisia zako.
Kwa akina dada nao, kwa nini ukubali kudanganyika eti kwa vile mtu amekuambia anakupenda? Tuwe makini kutamka neno hili na tutafakari jinsi ya kulipokea.

TEMBELEA BLOG HII KILA SIKU UPATE HEKIMA KUTOKA JUU MBINGUNI.

ASOMAYE NA AFAHAMU

(ASOMAYE NA AFAHAMU) Mathayo 24:15

Kitabu cha Danieli kinahusu nyakati zetu hizi za mwisho.
Kuelewa mambo yaliyo mbele yetu ni muhimu sana, maana ama
tutapata uzima wa milele, ama mauti ya milele katika mkabala
wetu na matukio hayo yanayokuja. Hivyo si suala dogo kujifunza
unabii wa kitabu cha Danieli kwa wote wanaotaka uzima wa milele.
Yesu akizungumza na wanafunzi wake juu ya matukio ya siku za
mwisho alisema, "Basi hapo mtakapoliona Chukizo la Uharibifu,
lile lililonenwa na Danieli, limesimama mahali patakatifu
(asomaye na afahamu)". Mathayo 24:15. Hatari kubwa i mbele
yetu! Yesu anataka kila asomaye alifahamu Chukizo hilo la
Uharibifu linalokuja ili atakapoliona akimbie kuokoa maisha yake
(Mt. 24:16-22). Chukizo la Uharibifu limetajwa mahali patatu
katika kitabu cha Danieli (Dan. 9:26,27; 11:31; 12:11). Lina
majina mengi katika kitabu cha Danieli na cha Ufunuo ----- Pembe
Ndogo, Mnyama, na kadhalika. Utashangaa kujua kwamba "mnyama"
katika lugha ya taaluma ya unabii sio tusi wala kashfa kama
wengi wanavyodhani. Maana yake ni "mfalme au ufalme"
(Dan.7:17). Biblia inajitafsiri yenyewe!
Hivi maana ya "chukizo" ni nini? Soma 2 Wafalme 21:1-11 na
Kumbukumbu la Torati 18:9-14. Kumbe! Chukizo ni kuabudu
sanamu, kuwaomba wafu, kushughulika na mapepo, uchawi au
ushirikina, kuabudu jua na nyota za mbinguni, na kadhalika.
Mataifa, yaani, wapagani hufanya mambo hayo. Je! "uharibifu"
ni nini? Sio kuharibu vitu, bali ni kuwaangamiza, yaani, kuwaua
watu (Dan.8:24,25). Kwa hiyo, Chukizo la Uharibifu ni mamlaka
au utawala au ufalme unaoabudu sanamu, unaowaomba wafu, ulio na
ushirikina, na, zaidi ya hayo, unaowaangamiza "watakatifu",
yaani, "hao wazishikao Amri [Kumi] za Mungu na Imani ya Yesu
(Ufu.14:12; Kut. 20:3-17; Yak. 2:10-12). Paulo analiita "mtu
wa kuasi, mwana wa uharibifu [mwuaji], mpingamizi [au Mpinga
Kristo] (2 The. 2:3,4].
Bila kila mtu kumjua huyo, Yesu Kristo hawezi kuja duniani.
Tutaendelea kusumbuka na magonjwa, umaskini, na dhiki. Je! si
jambo la muhimu kabisa kuijua mamlaka hiyo ili kujua la kufanya
kuokoa maisha yetu, si yale ya kimwili, bali ya kiroho ili
tupate kuishi milele? (Mt. 10:26-33; Yoh.6:39-40; Ufu.12:11).
Kufa au kutokufa si hoja, bali kujiweka tayari kumlaki Yesu
Kristo atakapokuja juu ya mawingu ya mbinguni (Ufu. 2:10; Mt.
24:29-31).
Mpendwa Msomaji, je! kwa neema yake Mungu unataka kuwa
tayari kujiunga na watakatifu ulimwenguni kote? Soma Danieli,
na ufahamu. Kabla hujaanza kusoma somo, omba ili Mungu akupe
Roho wake atakayekufundisha kweli yote (Yohana 16:13-15). Mungu
na akubariki!

ENDELEA KUTEMBELEA BLOG HII KILA SIKU UJUE MANENO YA UNABII

JE AGANO LA KALE LINA HABARI ZA YESU?

SWALI: 
NI NANI ALIYEFUNULIWA KATIKA MAANDIKO MATAKATIFU YOTE?

JIBU: 
YESU KRISTO,
 "Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake;na hayo ndiyo yanayonishuhudia" Yoh.5:39.
 Biblia nzima ni ufunuo wa kazi ya Kristo, hasa wa kazi yake ulimwenguni kwa ajili ya wanadamu. Kristo aliwafundisha wanafunzi wake juu yake mwenyewe kwa Maandiko ya Agano la Kale."Akaanza kutoka Musa na manabii wote,akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe" Luka 24:27.

FAHAMU KWAMBA:
YESU KRISTO WA NAZARETH NDIYE NJIA,KWELI NA UZIMA.YEYOTE AJAE KWAKE ATAPATA MAJI YA UZIMA BURE.

IJUE KWELI NAYO KWELI ITAKUWEKA HURU! BIBLIA YOTE KUANZIA KITABU CHA MWANZO HADI KITABU CHA UFUNUO NI NENO LA KRISTO NA NENO LAKE NDIYO KWELI.

SWALI:
 Mwalimu mwema nifanye nini ili ni uridhi UFALME WA MUNGU?

JIBU:

Yesu akajibu, Je,wazijua AMRI?Soma Kutoka 20:1-17(AMRI KUMI ZA MUNGU). Kijana akajibu Hizo nimezishika toka utoto wangu.
 Yesu akampenda akamwambia Kauze mali zako uwape maskini kisha unifuate.

FAHAMU KWAMBA:
 INATUPASA KUZISHIKA AMRI ZA MUNGU NA KUMFUATA KRISTO ILI TUWEZE KU URIDHI UFALME WA MUNGU (ku upata uzima wa milele)

TAFUTENI KWANZA UFALME WA MUNGU NA HAKI YAKE NA MENGINE MTAZIDISHIWA.

TEMBELEA BLOG HII KILA SIKU UJIFUNZE MAMBO MUHIMU ILI UWEZE KUPATA UZIMA WA MILELE
"Basi, enendeni,kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi,.. mkiwafundisha kushika yote niliyowaamuru ninyi: na tazama,mimi nipo pamoja nanyi siku zote,hata mwisho wa dunia" Alisema Bwana wetu.